Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Pili

6. Sukutuwa mdomo na weka maji puwani kwa pamoja mara tatu.

Njia ya kusukutua mdomo na upandishaji wa maji puani ni ifuatayo: kwanza, chukuwa maji katika kiganja cha mkono wa kulia. Alafu tumia baadhi ya maji, sukutua mara moja. Baada ya hapo tumia yaliyobaki kiganjani pandisha maji puani. Hii njia utairudia mara mbili, kwa kutumia kiganja kingine cha maji kila mara.

Soma Zaidi »

Kupata Qiraat Moja Ya Thawabu

Sayyidina Ally Bin Abii Taalib (radhiyallahu 'anhu) anaripoti kuwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema, "yoyote atakae niswalia mara moja, Allah subhaana wata'alah atamuandikia kirati moja ya thawabu, na kirati moja ni sawa na mlima wa uhudi.

Soma Zaidi »

Kupata Thawabu Sabini

Sayyidina Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu 'anhuma) alitowa ripoti, "Yoyote atakaye tuma salaam kwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) mara moja Allah subhaana wata'alah na malaika wake watatuma sabini rehema na baraka juu yake kwa kulipa salaam moja yake. Kwahivyo yoyote atakaye taka kuzidisha kumsaliya Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) azidishe kumsaliya Nabii. Na yoyote atakaye kuwa ataki kuzidisha kumsaliya Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) asizidishe kumsaliya Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) (yaani kama anataka kupata ujira mwingi,ni lazima azidishe kumsaliya Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam)).

Soma Zaidi »

Kupata Rehma Kumi

Sayyiduna Abu Huraira (radhiyallahu 'anhu) ameripoti kuwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema " yoyote atakaye nitumia salaam mara moja, allah subhaana wata'alah atamtumia salaam (yaani atampa zawadi na atamfariji na rehema zake) kwake mara kumi" 

Soma Zaidi »

Bashara Nzuri Kutoka Kwa Allah( Subhaanahu Wata’alah) Kwa Wale Ambao Wanamsalia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Hazrat Abdur Rahmaan Bin Auf (radhiyallahu 'anhu) alitowa taarifa kuwa kuna wakati mmoja, nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) alitoka nyumbani kwake na mimi nikamfuata, mpaka akaingia kwenye shamba la tende na hakashuka chini kusujudu. Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) alifanya sajida ndefu mpaka ni kaogopa kuwa mwenyezi mungu tayari amesha mchukuwa.

Soma Zaidi »

Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Pili

4. Osha mikono yote mpaka kwenye vifundo mara tatu

Sayyidina Humraan (rahimahullah), mtumwa aliye huru wa Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu)aliomba aletewe maji (kuonyesha watu jinsi gani ya kuchukuwa udhu). Kisha alianza kutawadha kwa kuosha mikono (mpaka kwenye vifundo) mara tatu. (kwenye riwaya hii, iliyopatikana ndani ya Sahihi Bukhari, Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kasema ” nilimuona Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) anafanya udhu kwa namna hii.)”

Soma Zaidi »