Sahaabah

Madai Ya Baadhi Ya Watu Wa Kufah:

Katika mwaka wa 21 A.H., baadhi ya watu wa Kufah walikuja kwa ‘Umar (Radhiyallahu ‘anhu) na kumlalamikia Sa’d (Radhiyallahu ‘anhu) kwamba hakuswali sawa sawa. Wakati huo, Sa’d (Radhiya Allahu ‘anhu) alichaguliwa na Umar (radhiyallahu ‘anhu) kama gavana wa Kufah. Hivyo basi ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwita Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) …

Soma Zaidi »

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwatuma katika mwaka wa kwanza baada ya Hijrah kuuzuia msafara wa Maquraishi. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimteua Ubaidah bin Haarith (radhiya allaahu ‘anhu) kuwa Amir (kiongozi) wa kundi hili. Katika msafara huu, Maswahabah (radhiyallahu ‘anhum) …

Soma Zaidi »

Damu Ya Kwanza iliyomwagika kwa ajili ya Uislamu

Muhammad bin Ishaaq (rahimahullah) anasimulia: Mwanzoni katika Uislamu, Maswahaabah wa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) walikuwa wakiswali kwa siri. Walikuwa wakienda kwenye mabonde ya Makka Mukarramah kuswali ili Swalah zao zibaki siri kwa makafiri (na ili waokoke na mateso ya makafiri). Wakati mmoja, wakati Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwepo pamoja na …

Soma Zaidi »

Upendo Kwa Answaar

‘Aamir (rahimahullah), mtoto wa Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu), anasimulia yafuatayo: Wakati fulani nilimwambia baba yangu, “Ewe baba yangu mpendwa! Ninaona kwamba unaonyesha upendo na heshima ya ziada kwa Answaar ikilinganishwa na watu wengine.” Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) akaniuliza, “Ewe mwanangu! Hujafurahishwa na hili?” Nikamjibu, “Hapana! Sina furaha. Lakini, nimefurahishwa sana …

Soma Zaidi »

Utabiri Wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuhusiana na Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) Kushinda Qaadisiyyah

Katika tukio la Hajjatul Wadaa’, Sa’d (Radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameumwa huko Makka Mukarramah na alihofia kwamba angeaga dunia. Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokuja kumtembelea, alianza kulia. Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akamuuliza: “Kwa nini unalia?” Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Nahofia kuwa nitafariki katika ardhi ambayo niliifanya Hijrah, na kwa kufariki …

Soma Zaidi »

Uthabiti wa Sa’d (Radhiyallahu ‘anhu) Kwenye Imaan Yake

Abu ‘Uthmaan (Rahimahullah) anasimulia kwamba Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema: Aya ifuatayo ya Qur’an tukufu iliteremshwa kunihusu mimi: وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا ۖ وَإِن جَاهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا Tumemuusia mwanaadamu kuwafanyia wema wazazi wawili. Na wakikulazimisha (wazazi wako makafiri) kunishirikisha (katika ibada yangu) yale …

Soma Zaidi »

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) Akimlinda Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

‘Aaishah (radhiya allaahu ‘anha) anasimulia: Baada ya hajiria Madinah Munawwarah, katika tukio moja, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hakupata usingizi usiku (kwa kuhofia kwamba maadui wangemshambulia). Hapo ndipo Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliposema: “Laiti kungekuwa na mchamungu wa kunilinda usiku huu.” Tukiwa katika hali hiyo, tulisikia milio ya silaha. Rasulullah (sallallahu …

Soma Zaidi »

Du’aa Maalum Ya Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam):

‘Aaishah binti Sa’d (radhiya allaahu ‘anha), binti wa Sa’d (radhiya Allaahu ‘anhu) ‘anhu), anasimulia yafuatayo kutoka kwa baba yake, Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu): Wakati wa Vita vya Uhud, (wakati maadui waliposhambulia kutoka nyuma na Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum) wengi wakauawa kwenye uwanja wa vita,) Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum) hawakuweza kumpata …

Soma Zaidi »

Ndoto Ya Sa’d (radhiyallahu ‘anhu) Kabla ya Kusilimu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba: Kabla ya kusilimu, niliota ndoto ambayo niliona niko gizani kabisa na kutokuona chochote. Ghafla, mwezi ukatokea ambalo ulianza kumulika usiku. Kisha nikaufuata huo mwanga hadi nikaufikia mwezi. Katika ndoto, niliona watu fulani ambao walikuwa wamenitangulia kuufikia mwezi. Nilimuona Zaid bin Haarithah, ‘Ali bin Abi …

Soma Zaidi »