
Imam Bayhaqi (rahimahullah) anasimulia:
Wakati Yazid bin Abi Sufyan (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa waziri wa Shaam, Waislamu walijishughulisha na Jihaad na kupata ushindi, na hivyo kuwa na ngawira.
Miongoni mwa ngawira za vita alikuwemo mtumwa mrembo aliyejikuta kwenye milki ya mwanajeshi mmoja wa Kiislamu. Muda mfupi baada ya yule mwanajeshi Mwislamu kumpokea kama milki yake ya ngawira, Yazid bin Abi Sufyaan (Radhiya Allaahu ‘anhu), kamanda wa jeshi, alikuwa amemchukua kwa ajili yake binafsi kutoka kwa yule mwanajeshi.
Wakati huo, Abu dhar Ghifaari (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwepo Shaam na mwanajeshi huyu alikwenda kwake kuomba msaada wa kumrejesha yule mtumwa kutoka kwa Yazid bin Abi Sufyaan (Radhiyallahu ‘anhu).
Hivyo, Abu dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu), akimchukua mwanajeshi huyo pamoja naye, wakaenda kwa Yazid bin Abi Sufyaan (Radhiyallahu ‘anhu) na akamuamrisha mara tatu amrudishe mtumwa huyo kwa mwanajeshi.
Abu dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia: “Tazama! Wallahi! Ukimtoa mtumwa huyu kutoka kwa mwanajeshi bila ya haki, basi jua kabisa kwamba nimemsikia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akisema, ‘Mtu wa kwanza kubadili Sunnah yangu atakuwa ni mtu katika kabila la Banu Umayyah.’” (na katika baadhi ya riwaya, pia imetajwa kuwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema “Mtu kutoka kwa Banu Umayyah ambaye atabadilisha sunna yangu, jina lake ni Yazid.” Musnad Abi Ya’la #871).
Akisema hivi, Abu dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aligeuza mgongo wake na kuondoka. Yazid bin Abi Sufyaan (Radhiyallahu ‘anhu) mara moja akamrudisha yule mtumwa kwa yule mwanajeshi na akaenda nyuma ya Abu dhar (Radhiyallahu ‘anhu) akimuuliza, “Nakuomba kwa jina la Mwenyezi Mungu! Tafadhali niambie, unadhani mimi ndiye mtu ambaye Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amemtaja katika Hadith hii?” Abu dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Hapana, wewe si mtu huyo.”
Baada ya kusimulia tukio hilo hapo juu, Imaam Bayhaqi (rahimahullah) alitaja, “Yazid bin Abi Sufyaan (Radhiya Allaahu ‘anhu), Swahaabi wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), alikuwa kiongozi wa jeshi la Shaam katika zama za Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) na ‘Umar (Radhiyallahu ‘anhu). Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alipomtaja mtu kutoka kwa Banu Umayyah kubadilisha Sunnah yake, Yazid bin Abi Sufyaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakukusudiwa (kwa sababu alikuwa Sahaabi wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na akaishi maisha ya haki kuafikiana na Sunnah).
Hata hivyo, Imaam Bayhaqi (rahimahullah) anaeleza zaidi kwamba kulikuwa na mtu mwingine kutoka kwa Banu Umayyah ambaye alikuwa na jina sawa. Alikuwa ni Yazid bin Mu‘aawiyah, mtoto wa Mu‘aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu), na inaonekana kuwa yeye ndiye aliyetajwa katika Hadith ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) (kwa sababu yeye ndiye alikuwa sababu ya kuleta madhara makubwa ndani ya Uislamu wakati wa utawala wa Banu Umayyah). (Dalaa’il-un-Nubuwwah 6/410)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu