Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akimuua Abu Jahl

Baada ya vita ya Badr na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na maswahaabah (Radhiyallahu anhum) walipata ushindi, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliwaambia Maswahaba, “Ni nani atakayekwenda kuona hali ya Abu Jahl?”

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikwenda kumtafuta na akakuta watoto wawili wa ‘Afraa (Radhiya Allaahu ‘anha) wamemumiza na akiwa katika sakaratil maut.

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuja kwake na kuweka mguu wake kwenye shingo lake. Akazishika ndevu zake pia na akamwambia: ” Je wewe ni Abu Jahl? Ewe adui wa Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu amekufedhehesha!”

Abu Jahl akajibu: “Je, kuna mtu mkubwa kuliko mimi ambaye nyinyi mmemuua?” Vile vile alimwambia Abdullah bin Mas’uud, “Ewe mchungaji mdogo! wewe unajaribu kupanda mlima mkubwa na mgumu (hadi kwenye hali ha kifo bado anaonyesha kiburi wa hali ya juu)

Baada ya hapo, akasema: “Lau kama mtu asiyekuwa mkulima kama wewe angeweza kuniua (ili ingekuwa ni heshima kwangu).”

Abu Jahl pia alimwambia Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu anhu): “Unaponikata kichwa, basi ukate kichwa changu kutoka chini ya shingo langu, karibu na bega langu, ili watu watakapotazama kichwa changu, kitashangaza zaidi (na kuwa juu zaidi kuliko vichwa vya wengine kwenye jeshi letu ambao wameuwawa).”

Vile vile alimwambia Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu), “Utakaporejea kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), basi mwambie kwamba mimi nimesema: “Chuki yangu kwako leo ni zaidi kuliko nilikuwa nikikuchukiya zamani. Vile vile, katika maisha yangu yote, siku zote nilibaki kuwa adui wa Allah Ta’ala, lakini leo uadui wangu kwa Allah Ta’ala ni mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa zamani.”

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) kisha akamuua kwa kumkata kichwa na upanga wake. Kisha akakileta kichwa kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na akasema: “Hiki ni kichwa cha adui wa Mwenyezi Mungu, Abu Jahl.”

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliuliza kwa furaha, “Wallahi (hiki ni kichwa cha Abu Jahl)?”

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliapa kwa jina la Allah akisema: “Hiki ni kichwa cha Abu Jahl, na Allah Ta’ala amenipa nguvu na uwezo wa kumuua.

Baada ya hapo Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akasema:

الله أكبر، الحمد الله الذي صدق وعده، ونصر عبده، وهزم الأحزاب وحده

Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa! Sifa njema zote ni za Allah Ta’ala! Ameitimiza ahadi yake, na amemsaidia mja wake, na amemshinda adui peke yake!

Baada ya hapo, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu), “Nionyeshe mwili wake ulipo.

Wakati Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipompeleka Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kwenye mwili wa Abu Jahl, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema maneno yafuatayo mara tatu:

الحمد الله الذي أعز الإسلام وأهله

Sifa zote njema anastahiki Allah Ta’ala, Ambaye peke yake Ameutukuza Uislamu na Watu wa Kiislamu

Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) pia akasema: “Huyu ndiye Fir’oun wa Ummah huu.”

Kisha Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akampa Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) upanga wa Abu Jahl (kama ngawira).

(Sahih Bukhaari #4020, Musnad Ahmad #4247 na Fat-hul Baari juzuu ya 7, 374)

About admin

Check Also

Kufariki Kwa Abu Dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Wakati Abu Dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokaribia mwisho wake, hapakuwa na mtu yoyote pamoja naye …