25. Usipasue vifundo vyako ukiwa msikitini. Vile vile, usiunganishe vidole vyako ukiwa umeketi msikitini.
Mtumwa aliyeachiliwa huru wa Sayyidina Abu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) anasema, “Siku moja, nikiwa na Abu Sa’eedd (radhiyallahu ‘anhu) na yeye akiwa pamoja na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), tuliingia msikitini na tukamuona mtu mmoja ameketi katikati ya musjid. Mtu huyu alikuwa amekaa kitako kwa jinsi magoti yake yalivyoinuliwa, na mikono yake ikiwa imezunguka magoti yake, na vidole vya mikono yake yote miwili vimeunganishwa. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliimpa ishara mtu huyu (kuvuta mazingatio yake), lakini mtu huyo hakuona ishara ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hivyo akageuka kumelekea Abu Sa’eed (radhiyallahu ‘anhu) na akasema, ‘Mmoja wenu atakapokuwa msikitini, basi asiunganishe vidole vyake, kwani kuunganisha vidole vyake ni kutoka kwa Shetani. Kwa muda utabakia msikitini mkingojea Swalaah, mtapata ujira wa Swalaah kama mko katika Swalaah mpaka mtakapotoka msikitini. Kuunganisha vidole wakati wa Swalaah ni kinyume na adabu ya Swalaah, basi mtu hatakiwi kuunganisha vidole wakati wa kusubiri Swalaah).’”
Soma Zaidi »