Sunna za Msikiti

25. Usipasue vifundo vyako ukiwa msikitini. Vile vile, usiunganishe vidole vyako ukiwa umeketi msikitini.[1] 

عن مولى لأبي سعيد الخدري قال بينا أنا مع أبي سعيد رضي الله عنه وهو مع رسول الله صلى الله عليه وسلم إذ دخلنا المسجد فإذا رجل جالس في وسط المسجد محتبيا مشبكا أصابعه بعضها في بعض فأشار إليه رسول الله صلى الله عليه وسلم فلم يفطن الرجل لإشارة رسول الله صلى الله عليه وسلم فالتفت إلى أبي سعيد فقال إذا كان أحدكم في المسجد فلا يشبكن فإن التشبيك من الشيطان وإن أحدكم لا يزال في صلاة ما كان في المسجد حتى يخرج منه (مجمع الزوائد، الرقم: 2047 ، الترغيب والترهيب، الرقم: 450)

Mtumwa aliyeachiliwa huru wa Sayyidina Abu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) anasema, “Siku moja, nikiwa na Abu Sa’eedd (radhiyallahu ‘anhu) na yeye akiwa pamoja na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), tuliingia msikitini na tukamuona mtu mmoja ameketi katikati ya musjid. Mtu huyu alikuwa amekaa kitako kwa jinsi magoti yake yalivyoinuliwa, na mikono yake ikiwa imezunguka magoti yake, na vidole vya mikono yake yote miwili vimeunganishwa. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliimpa ishara mtu huyu (kuvuta mazingatio yake), lakini mtu huyo hakuona ishara ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hivyo akageuka kumelekea Abu Sa’eed (radhiyallahu ‘anhu) na akasema, ‘Mmoja wenu atakapokuwa msikitini, basi asiunganishe vidole vyake, kwani kuunganisha vidole vyake ni kutoka kwa Shetani. Kwa muda utabakia msikitini mkingojea Swalaah, mtapata ujira wa Swalaah kama mko katika Swalaah mpaka mtakapotoka msikitini. Kuunganisha vidole wakati wa Swalaah ni kinyume na adabu ya Swalaah, basi mtu hatakiwi kuunganisha vidole wakati wa kusubiri Swalaah).’”

26. Usichafue Msikiti k.m. kwa kutema mate msikitini au kupuliza pua na kuruhusu uchafu uanguke chini.[2]

عن أبي ذر رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم عرضت علي أعمال أمتي حسنها وسيئها فوجدت في محاسن أعمالها الأذى يماط عن الطريق ووجدت في مساوئ أعمالها النخاعة تكون في المسجد لا تدفن (صحيح مسلم، الرقم: 553)

Sayyidina Abu Zar (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kasema, “Amali njema na maovu ya Ummah wangu ziliwasilishwa mbele yangu. Niliona kuwa miongoni mwa wema ni mtu kuondosha kitu chenye madhara kwenye njia, na nikaona Miongoni mwa maovu ni (ya mtu kuacha) uchafu wa pua (ulioanguka chini) ndani ya Msikiti bila kuzika.”

عن أنس رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم البزاق في المسجد خطيئة وكفارتها دفنها (صحيح البخاري، الرقم: 415)

Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Akasema: “Kutemea mate msikitini ni dhambi, na malipo yake ni kuuzika (na mchanga). (Hii ilikuwa ni wakati ambapo Swalaah msikitini ilikuwa inaswaliwa kwenye ardhi tupu.)


[1] اتفق الأصحاب على كراهة تشبيك الأصابع في طريقه إلى المسجد وفي المسجد يوم الجمعة وغيره، وكذا سائر أنواع العبث ما دام في الصلاة أو منتظرها لأنه في صلاة (المجموع شرح المهذب 4/391 ، مغني المحتاج 1/652)

ولا يشبك بين أصابعه ولا يفرقع في الطريق ولا في المسجد كما لا يفعل في الصلاة (التهذيب في فقه الإمام الشافعي 2/351)

[2] قال المصنف رحمه الله (وان بدره البصاق فان كان في غير المسجد لم يبصق تلقاء وجهه ولا عن يمينه بل يبصق تحت قدمه اليسرى أو عن يساره وإن بدره في المسجد بصق في ثوبه وحك بعضه ببعض (المجموع شرح المهذب 4/25)

About admin

Check Also

Sunna Za Msikiti

27. Uwe mtulivu na mwenye heshima ukiwa msikitini, wala usighafilike na kusahau heshima ya msikiti. …