Sunna Za Msikiti

31. Mbali na kwenda msikitini kuswali, ikiwa kuna shughuli inayofanyika msikitini, basi mtu aweke nia ya kwenda msikitini kupata elimu ya Dini. Ikiwa mtu ana uwezo wa kufundisha Dini basi afanye nia ya kuja msikitini ili kuwapa watu elimu ya Dini ikiwa atapata fursa ya kufanya hivyo.

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول من جاء مسجدي هذا لم يأته إلا لخير يتعلمه أو يعلمه فهو بمنزلة المجاهد في سبيل الله ومن جاء لغير ذلك فهو بمنزلة الرجل ينظر إلى متاع غيره (سنن ابن ماجة، الرقم: 227)[1]

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ametaja: “Nilimsikia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akisema: “Yoyote anayekuja kwenye msikiti wangu huu, na haji kwa lengo lolote isipokuwa kujifunza kheri au kufundisha mema, basi anakuwa kama yule anayejitoa katika njia ya Allah Ta’ala, na anayekuja msikitini kwa madhumuni mengine (isipokuwa ibada ya Allah Ta‘ala), basi huyo ni kama mtu anayetazama biashara ya wengine (yakiuzwa, lakini hapati kitu).

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من أتى المسجد لشيء فهو حظه (سنن أبي داود، الرقم: ٤٧٢)[2]

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema: “Mwenye kufika msikitini kwa makusudio fulani, basi hilo litakuwa fungu lake (yaani atalipwa kwa nia yake).”

32. Pamoja na kuuweka Msikiti kuwa safi, pia weka msikiti kuwa na harufu nzuri kwa kuchoma udi, nk.

عن عائشة رضي الله عنها قالت أمر رسول الله صلى الله عليه وسلم ببناء المساجد في الدور وأن تنظف وتطيب وقال سفيان قوله ببناء المساجد في الدور يعني القبائل (سنن الترمذي، الرقم: ٥٩٤)[3]

Sayyidatuna Aa’ishah (radhiyallahu ‘anha) anaripoti kwamba Sayyiduna Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) aliamuru kwamba misikiti ijengwe katika maeneo mbalimbali, na kwamba misikiti hiyo iwe safi na iwe na manukato.”

عن ابن عمر رضي الله عنهما أن عمر بن الخطاب رضي الله عنه كان يجمر المسجد في كل جمعة (مصنف ابن أبي شيبة، الرقم : 7523)

Sayyidina Abdullah bin Umar (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Sayyiduna Umar (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa akichoma udi kwenye msikiti siku ya Ijumaah.


[1] قال البوصيري في الزوائد (1/83): إسناده صحيح على شرط مسلم

[2] قال المنذري: في إسناده عثمان بن أبي العاتكة الدمشقي وقد ضعفه غير واحد (مختصر سنن أبي داود 1/194)

قال الذهبي: في ميزان الإعتدال (5/53) تحت ترجمة عثمان بن أبي العاتكة قال أحمد لا بأس به

[3] قال المنذري: رواه أحمد والترمذي وقال حديث صحيح وأبو داود وابن ماجه وابن خزيمة في صحيحه ورواه الترمذي مسندا ومرسلا وقال في المرسل هذا أصح (الترغيب والترهيب، الرقم: 432)

About admin

Check Also

Sunna za Msikiti

25. Usipasue vifundo vyako ukiwa msikitini. Vile vile, usiunganishe vidole vyako ukiwa umeketi msikitini.

Mtumwa aliyeachiliwa huru wa Sayyidina Abu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) anasema, “Siku moja, nikiwa na Abu Sa’eedd (radhiyallahu ‘anhu) na yeye akiwa pamoja na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), tuliingia msikitini na tukamuona mtu mmoja ameketi katikati ya musjid. Mtu huyu alikuwa amekaa kitako kwa jinsi magoti yake yalivyoinuliwa, na mikono yake ikiwa imezunguka magoti yake, na vidole vya mikono yake yote miwili vimeunganishwa. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliimpa ishara mtu huyu (kuvuta mazingatio yake), lakini mtu huyo hakuona ishara ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hivyo akageuka kumelekea Abu Sa’eed (radhiyallahu ‘anhu) na akasema, ‘Mmoja wenu atakapokuwa msikitini, basi asiunganishe vidole vyake, kwani kuunganisha vidole vyake ni kutoka kwa Shetani. Kwa muda utabakia msikitini mkingojea Swalaah, mtapata ujira wa Swalaah kama mko katika Swalaah mpaka mtakapotoka msikitini. Kuunganisha vidole wakati wa Swalaah ni kinyume na adabu ya Swalaah, basi mtu hatakiwi kuunganisha vidole wakati wa kusubiri Swalaah).’”