Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) akiwa katika jukumu la kutunza mkuki wa Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam)

Mfalme wa Abyssinia (Najaashi (Rahimahullah) aliwahi kumtumia Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) mikuki mitatu kama zawadi. Baada ya kupokea mikuki mitatu, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) aliimpa Ali (Radhiyallahu’ Anhu) mkuki mmoja, akaampa Umar (Radhiyallahu’ Anhu) mkuki wa pili na akabaki na mkuki wa tatu.

Katika vipindi vya laidi (idi ndogo na idi kubwa), Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alikuwa akibeba mkuki wa Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) na kutembea mbele yake. Alikuwa akitembea mbele ya Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) wakati akiwa ameshikilia mkuki kwa kumheshimu Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam).

Wakati Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) na Bilaal (Radhiyallahu ‘anhu) wakifika katika uwanja wa kuswali, Bilaal (Radhiyallahu Anhu) alikuwa akiweka ule mkuki kwenye ardhi ili iwe kama sutra wakati akiswali swalah ya idi.

Baada ya Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) kuondoka duniani na Abu Bakr (Radhiyallahu’ Anhu) akawa Khalifah, Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alikuwa akifanya hivyo hivyo kwa Abu bakr (Radhiyallahu anhu) katika zile laidi mbili. (Siyar A’laam Nubalaa ‘3/221)

About admin

Check Also

Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) Akitoa Adhaan Juu Ya Ka’bah Shareef

Katika hafla ya Fath-ul-Makkah (ushindi wa Makkah), Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) aliingia ndani ya Ka’bah …