Monthly Archives: May 2022

Fadhila za Mwenye kwenda kwenye Msikitini Kutekeleza Swalaah

4. Kuenda msikitini mara Kwa mara ni njia ya usalama kwa Imaan na Dini ya mtu.

Sayyiduna Mu’aaz bin Jabal (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema: "Hakika Shaitaan ni mbwa mwitu wa mwanadamu (anayemuwinda mtu), kama jinsi mbwa mwitu wa mbuzi anayemkamata mbuzi aliye mbali na kujitenga na kundi. Jiepusha na kuishi kwa kujitenga kwenye tambarare (au kujiepusha na maoni yaliyotengwa) na kushikilia kwa uthabiti wa Ahlus Sunnah wal Jamaa’ah na kubaki na ummah walio wengi na kushikamana na msikiti.”

Soma Zaidi »

Fadhila za Mwenye kwenda Msikitini Kutekeleza Swalaah

1. Kufanya udhu nyumbani na kutembea kwenda msikitini kuswali ni njia ya mtu kusamehewa madhambi yake na daraja lake kuinuliwa.

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema, “Mwenye kutawadha nyumbani na baada ya hapo kutembea kuelekea kwenye nyumba miongoni mwa nyumba za Allah (subhaana wata'ala) ili akamilishe faradhi ya Allah (subhaana wata'ala), Basi Kwa kila hatua moja anachukuwa, dhambi moja inasamehewa, na kwa hatua inayofuata, atainuliwa daraja moja."

Soma Zaidi »

Kumswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kabla ya kusoma Dua

Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) amesema “Wakati wowote mtu kati yenu akikusudia kumwomba Allah (subhaana wata'ala), Basi aanze dua yake kwa kumhimidi na kumtakasa Allah (subhaana wata'ala) kwa sifa zinazostahiki Utukufu na heshima yake. Kisha amtumie salaa na salaam juu ya Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na baada ya hapo aombe dua, Kwa sababu (kupitia kufuata njia hii ya kuomba dua) kuna uwezekano mkubwa kwamba atakuwa amefanikiwa (katika dua yake kujibiwa)."

Soma Zaidi »

Fadhila za Musjid

1. Misikiti imetangazwa kuwa ndio sehemu inayopendwa zaidi kwa Allah subhaana wata’ala. عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال أحب البلاد إلى الله مساجدها وأبغض البلاد إلى الله أسواقها (صحيح مسلم، الرقم: 671) Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu …

Soma Zaidi »