Fadhila za Musjid

1. Misikiti imetangazwa kuwa ndio sehemu inayopendwa zaidi kwa Allah subhaana wata’ala.

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال أحب البلاد إلى الله مساجدها وأبغض البلاد إلى الله أسواقها (صحيح مسلم، الرقم: 671)

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema, “Sehemu zinazopendwa sana zaidi kwa Allah (subhaana wata’ala) ni Misikiti, na sehemu zinazochukiwa sana zaidi kwa Allah subhaana wata’ala ni sokoni.”

2. Mtu akijenga msikiti kwa ajili ya Allah (subhaana wata’ala), basi Allah (subhaana wata’ala) atamjengea jumba kubwa kati ya Jannah.

عن عبيد الله الخولاني يذكر أنه سمع عثمان بن عفان رضي الله عنه عند قول الناس فيه حين بنى مسجد الرسول صلى الله عليه وسلم إنكم قد أكثرتم وإني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول من بنى مسجدا لله تعالى قال بكير حسبت أنه قال يبتغي به وجه الله بنى الله له بيتا في الجنة (صحيح مسلم، الرقم: 533) وفي رواية أخرى بني له بيت أوسع منه في الجنة (مسند أحمد، الرقم: 7056)[1]

Ubaidullah Khawlaani (rahimahullah) anaripoti kwamba alimsikia Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kusema, wakati ambapo watu walimpinga (kufanya mabadiliko makubwa wakati wa kupanua msikiti wa Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), kama vile kutumia mbao za teak na matofari ya kuoka)“Hakika nyinyi watu mmepinga kuongezwa kwangu mara nyingi. Na nilimsikia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akisema, ‘Mwenye kujenga msikiti kwa ajili ya Allah Ta‘ala , kwa kutaka radhi za Allah (subhaana wata’ala) Basi Allah (subhaana wata’ala) atamjengea kasri kati ya Jannah. Kwa mujibu wa Hadith nyingine, mtu anayejenga msikiti kwa ajili ya Allah Ta‘ala atapokea kasri kati ya Jannah ambayo ni kubwa na pana zaidi kuliko msikiti alioujenga.


[1] قال المنذري في الترغيب (الرقم: 419): رواه أحمد بإسناد لين لهذا الحديث شاهد من حديث عبد الله بن عمرو قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من بنى لله مسجدا بنى الله له بيتا أوسع منه في الجنة رواه أحمد وفيه الحجاج بن أرطاة وهو متكلم فيه (مجمع الزوائد، الرقم: 1935)

وله شاهد آخر من حديث أبي أمامة قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من بنى لله مسجدا بنى الله له بيتا في الجنة أوسع منه رواه الطبراني في الكبير وفيه علي بن يزيد وهو ضعيف (مجمع الزوائد، الرقم: 1946)

About admin

Check Also

Fadhila za Jumu’ah

Kusamehewa Madhambi Kwa Kuswali Jumu’ah Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu …