CREATOR: gd-jpeg v1.0 (using IJG JPEG v80), default quality

Kusafiri

Dini ya Uislamu imewasilisha sheria na maamrisho, na sunna na adabu, ili kumfundisha mwanadamu jinsi ya kuishi katika hali zote.

Kama vile Dini ya Uislamu imetoa muongozo kwa mtu anapokuwa katika mji wake, vivyo hivyo imempa muongozo wa namna ya kujishughulisha anapokuwa safarini.

Kwa maneno mengine, Dini ya Uislamu ni kamili, pana ambayo inazingatia wakati wote na hali zote na kumpatia mwongozo ufaao.

Kwa hivyo, tunaona kwamba Shariah imetoa idhini kwa mtu anayesafiri kuswali rakaa mbili badala ya rakaa nne. Vile vile Shariah imetoa idhini kwa msafiri kutofunga Ramadhaan, na badala yake kufunga qadhaa zilizokoswa baada ya mwezi wa Ramadhaan.

Inajulikana kuwa mtu anaposafiri basi nyakati fulani huwa ananyimwa usingizi na faraja ili kuharakisha safari na kufika anakoenda kwa wakati. Vile vile, wakati mwingine, yeye anakabiliwa na hali ambazo ni kinyume na tabia yake na asili. Anaweza kulazimika kutokula chakula na vinywaji kwa kiwango cha maisha ambayo amezoea katika mji wake wa asili, ili kutimiza tu kusudi la safari yake.

Hivyo basi, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) ametuusia kwamba baada ya mtu kutimiza lengo la safari yake, arudi nyumbani. Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Kusafiri ni kama sehemu ya Jahannum ambayo humzuia mtu asipate chakula, kinywaji na usingizi wake (yaani, kusafiri kunaleta shida, kama vile mtu anavyopata shida ndani ya Jahannum). Hivyo, mtu anapomaliza kusudi na kazi ya safari, anapaswa kuharakisha kurudi kwa familia yake.”

Kimsingi, Dini ya Uislamu imetoa sunna nyingi na aadaab ambazo mtu anapaswa kuzifanyia kazi wakati wa safari ili apate urahisi na faraja wakati wa safari na pia kuwa chanzo cha rehema kwa wengine.

About admin