CREATOR: gd-jpeg v1.0 (using IJG JPEG v80), default quality

Sunna Na Adabu Kusafiri 1

1. Kabla ya kuanza safari (yaani kusafiri kwenda sehemu ambayo ni kilomita 78 au zaidi), mtu anatakiwa kuswali rakaa mbili. Swalaah hii inajulikana kama Swalaatus Safar.

Mut’im bin Miqdaam (rahimahullah) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Hakuna kitendo ambacho mtu anaweza kukiacha pamoja na familia yake kabla ya kuanza safari ambayo ni kheri zaidi kuliko rakaa mbili (Swalatus Safar) watakayoiswali.”

Imepokewa kwamba wakati wowote Ibnu Umar (Radhiyallahu anhuma) alipokusudia kuanza safari, alikuwa anaenda msikitini kwanza na kuswali.

2. Kutana na wanafamilia na marafiki zako kabla ya kuanza safari (kama unaposafiri kwa ajili ya umrah au hajj) na uwaombe wakuombee dua.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (Radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mmoja wenu anapotaka kusafiri basi anapaswa kukutana na ndugu zake Waislamu (yaani familia na marafiki na kuomba wamuombee dua). Hakika dua yao iliyoongezwa pamoja na dua yake itakuwa ni njia ya yeye kupata wema (wakati wa safari yake).

3. Wajulishe familia yako sehemu unapokwenda na mahali unapoishi wakati wa safari yako ili iwe rahisi kwao kuwasiliana nawewe.

4. Wakati wa kuondoka, soma dua ya masnoon ya safar:

بِسْمِ اللهِ اَلْحَمْدُ لِلّٰه سُبْحَانَ الَّذِيْ سَخَّرَ لَنَا هٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِيْنَ  وَإِنَّا إِلٰى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُوْنَ اَلْحَمْدُ لِلّٰه اَلْحَمْدُ لِلّٰه اَلْحَمْدُ لِلّٰه اَللهُ أَكْبَرُ اَللهُ أَكْبَرُ اَللهُ أَكْبَرُ لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ سُبْحَانَكَ اللّٰهُمَّ إِنِّيْ ظَلَمْتُ نَفْسِيْ فَاغْفِرْ لِيْ فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذُّنُوْبَ إِلَّا أَنْتَ

Kwa jina la Allah Ta’ala. Sifa zote njema ni za Allah Ta‘ala, Ametakasika Allah Ta’ala ambaye amemtiisha mnyama huyu (au akiweka gari hili chini ya udhibiti wetu) na hali sisi hatukuweza kulidhibiti (bila ya msaada Wake). Hakika sisi tutarejea kwa Mola wetu. Sifa njema zote ni za Allah Ta‘ala. Sifa njema zote ni za Allah Ta’ala. Sifa njema zote ni za Allah Ta‘ala. Allah Ta’ala ndiye mkubwa zaidi. Allah Ta’ala ndiye mkubwa zaidi. Allah Ta’ala ndiye mkubwa zaidi. Hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Ta’ala. (Ewe Mwenyezi Mungu subhaanahu wata’ala) Wewe ni mtakatifu zaidi. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, basi nisamehe, kwani hakuna anayesamehe madhambi isipokuwa Wewe.

5. Ni vyema kuanza safari siku ya Alhamisi. Kwa hivyo, ikiwa inawezekana kwako kusafiri siku ya Alhamisi, basi unapaswa kuanza safari yako siku ya Alhamisi. Kuanza safari siku nyingine yoyote pia inajuzu.

Ka’b bin Maalik (radhiyallahu anhu) alisema, “Ilikuwa ni tabia ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kwamba anapokusudia kuanza safari, kwa kawaida alikuwa akiondoka siku ya Alhamisi.

Ka’b bin Maalik (radhiyallahu anhu) alisema, “ Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliondoka siku ya Alhamisi kwa ajili ya vita vya tabuk, na alikuwa akipenda kuondoka siku ya Alhamisi.”

6. Hakikisha kuwa una mahitaji ya kutosha kwa ajili ya safari k.m. petroli, nguo, pesa za matumizi n.k.

Imepokewa kwamba Ibnu Umar (Radhiyallahu anhuma) alisema, “Ni sehemu ya heshima na utukufu wa mtu kwamba anachukua riziki za kutosha wakati wa safari yake.”

7. Ikiwa unawaacha wanaokutegemea k.m. mke na watoto n.k. basi kabla ya kuondoka, hakikisha kwamba mipango ya kutosha inafanywa ili mahitaji yao yatimizwe wakati wa kutokuwepo kwako.

About admin

Check Also

Kabla ya kulala, soma yafuatayo:

a) Tasbeeh-ul-Fatimi yaani Subhanallah mara 33, Alhamdulillah mara 33, Allahu Akbar mara 34 Ali (radhiyallahu …