a) Tasbeeh-ul-Fatimi yaani Subhanallah mara 33, Alhamdulillah mara 33, Allahu Akbar mara 34
Ali (radhiyallahu anhu) anaripoti: Wakati mmoja, Faatimah (Radhiyallahu anha) alienda nyumbani kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kulalamika kuhusu ugumu aliokuwa akiupata alipokuwa akitumia kinu. Habari zikamfikia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amepokea baadhi ya watumwa (hivyo alifikiria kumuomba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) mtomwa mmoja kumsaidia katika kazi zake za kila siku). Lakini, (baada ya kufika nyumbani,) hakumkuta Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), hivyo basi alimfahamisha Aaishah (radhiyallahu anha) sababu ya kumtembelea. Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alipofika nyumbani, Aaishah (radhiyallahu anha) alimfahamisha kuhusu swala hilo la Faatimah (Radhiyallahu anha). Baadaye, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuja nyumbani kwetu tulipokuwa tukitaka kulala. (Tulipomuona) tulikusudia kuamka (kwa kumheshimu), lakini Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akatuambia tubaki vile tulivyokuwa. Kisha akaja na kuketi kati yetu, mpaka nilipoweza kuhisi ubaridi wa miguu yake kwenye tumbo langu (kwa sababu ya yeye kuwa baina yetu na karibu nasi, miguu yake uliobarikiwa yaligusa ubavu wa mwili wangu). Kisha akasema, “Je, nisikuonyeshe kilicho bora zaidi kuliko ulichoomba (yaani bora kuliko mtumwa wa kukusaidia katika kazi zako za kila siku)? Kabla ya kulala, soma Subhanallah mara 33, Alhamdulillah mara 33 na Allahu Akbar mara 34, kwa sababu hakika hii ni bora kwako (katika kukusaidia katika kazi zako za kila siku) kuliko kupata mtumwa.” (Kwa mujibu wa riwaya nyingine,) Ali (Radhiyallahu anhu) akasema zaidi, “Sikuiacha tabia hii tangu nilipoisikia kutoka kwa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam ). Mtu mmoja aliyekuwepo aliuliza, “Hata katika usiku umya Siffeen (yaani usiku wa Vita vya Siffeen)?” Akajibu, “Hata usiku wa Siffeen.”
b) Ayatul Kursi
Ali (Radhiyallahu anhu) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kusoma Aayatul-Kursi usiku wakati wa kulala, Allah Ta’ala atailinda nyumba yake, nyumba za majirani zake, na nyumba za watu walio karibu naye.”
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu