Dua Ya kumi
لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْرٌ وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَاللهُ أَكْبَرُ
Hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah Ta’ala Peke Yake. Hana mshirika. Kwake yeye ni ufalme wote, na sifa njema zote ni zake, na Yeye ndiye Mwenye uweza wa kila kitu, na hakuna uwezo (wa kujiepusha na madhambi) na hakuna nguvu (ya kuyatenda matendo mema) isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala). Ametakasika Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) kwa sifa zake! Hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah, na Allah Ta’ala ndiye Mkubwa zaidi.
Kumbuka: Kupitia kusoma dua hii kabla ya kulala, madhambi yote ndogo ndogo yatasamehewa, hata kama ni nyingi zaidi kuliko povu la bahari.
Dua Ya Kumi na Moja
اَللّٰهُمَّ اغْفِرْ لِيْ وَاخْسَأْ شَيْطَانِيْ وَفُكَّ رِهَانِيْ وَثَقِّلْ مِيْزَانِيْ وَاجْعَلْنِيْ فِيْ النَّدِيِّ الْأَعْلٰى
Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala)! Nisamehe madhambi zangu, na niepushe na Shet’ani wangu (asinidhuru), na uniweke huru (na minyororo za madhambi), na ufanye mizani yangu (ya matendo mema) kuwa nzito (Siku ya Qiyaamah), na nisababishie kuwa miongoni mwa mkusanyiko wa waja wako wema na Malaika.
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu