Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) akiwa na yaqeen na Maneno ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam)

Wakati fulani, katika kipindi cha ukhalifa wake, Uthmaan (Radhiyalhu ‘anhu) alikuja kumtembelea Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu). Wakati huo, Abdullah bin Masoud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa na ugonjwa wake wa mwisho. Uthman (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuuliza, “Ni maradhi gani unayoyapata (ambayo yanakusababishia ugumu)?”

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Kitu ambacho kinanisababishia ugumu wakati huu ni wasiwasi wa kutowa hesabu za madhambi zangu mbele ya Allah Ta’ala.”

Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuuliza: “Je, una chochote unachokiitaji nikutimizie?” Akasema: “Kwa wakati huu ninachokitaka ni rehema ya Mola wangu.

Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) baadaye akamuuliza, “Je, nikupangie daktari akuhudumie?” Akajibu, “Daktari wa kweli (yaani Allah Ta’ala ambaye ana uwezo wa kuponya) ndiye ambaye amenisababishia maradhi.”

Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamuuliza, “Je, nisiagize utolewe posho kutoka kwenye hazina ya umma?” Akajibu, “Kwa wakati huu, sina haja nayo.”

Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema: “Huenda ikawa na faida kwa mabinti zako.” Abdullah bin Masuud (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema: “Je, mnaogopa umasikini utawasibu mabinti zangu? nimewausia wasoma Surah Waaqiah kila usiku, kwa sababu nilimsikia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akisema, ‘Mwenye kusoma Sura Waaqiah kila usiku, ufukara hautampata kamwe.’” ( Usdul Ghaabah 3/38)

About admin

Check Also

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa ni kijana mdogo, akikuwa akichunga mbuzi za Uqbah …