KUAMKA

Kabla ya kulala, tunafundishwa kusoma dua za masnoon na kumdhukuru Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah). Miongoni mwa dua za mchana kabla ya kulala ni dua ifuatayo:

اَللّٰهُمَّ بِاسْمِكَ أَمُوْتُ وَأَحْيٰى

Ee Mwenyezi Mungu, kwa jina lako nitakufa na kuishi.

Katika dua hii, usingizi umefanishwa na kifo, kutokana na ukweli kwamba wakati mtu analala, hupoteza hisia zake na fahamu.

Kwa hiyo, kutokana na dua hii, tunafundishwa kwamba wakati wa kulala, mtu ajitayarishe kukutana na Allah Ta‘ala.

Vile vile, wakati wa kuamka, moja ya dua za masnoon tulizo fundishwa kusoma ni:

اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ الَّذِيْ أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا وَإِلَيْهِ النُّشُوْرْ

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) aliyetujaalia uhai baada ya kufa na kwake Yeye tu ndio tutarejeshwa.

Katika dua hii, tunakumbushwa kwamba kupitia kuamka baada ya kula, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) ametupa tena fursa ya maisha.

Kadhalika, sisi pia tunakumbushwa kufufuliwa kwetu Siku ya Qiyaamah. Kwa maneno mengine, tunafundishwa kwamba tunapaswa kuchukua hii siku mpya katika maisha yetu kama baraka na fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) na tuitumie kujiandaa kwa ajili ya Siku ya Hukumu.

About admin