Muaz bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba katika tukio moja, Nabi (Sallallahu alaihi wasallam) alinishika mkono na kuniambia, “Ewe Muaz!”, na nikamjibu, “Nipo kwako kukuhudumia.”
Kisha Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akaniambia: “Hakika mimi nakupenda (kwa ajili ya Allaah Ta’ala).” Muaaz bin Jabal (Radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Na aapa kwa jina la Allah, mimi pia nakupenda.”
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Je, nikufundishe dua ya kusoma baada ya kila swalah.”
Muaaz (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema, “Ndio, (tafadhali nifundishe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu)”.
Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Ewe Muaaz! nakuusia kutokuacha kusoma dua hii baada ya kila swalah ya fardh:
اللهم أعني على ذكرك وشكرك وحسن عبادتك
Ewe Mwenyezi Mungu! Ninakuomba unisaidie kukukumbuka Wewe, kukushukuru na kukuabudu kwa wema.
(Al Adabul Mufrad #690 & Sunan Abi Dawood #1522)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu