Kusherehekea mwaka mpya

Swali: je inajuzu kutakiana “heri ya mwaka mpya” mwaka mpya wa kiingereza unapoanza? Baadhi ya watu wanasema kwamba sherehe ya mwaka mpya ina maana fulani ya ku kufuru. Je hii ni sahihi?

jibu: sherehe ya mwaka mpya ni sherehe ya “kidini” ya makafiri ambayo inahusishwa na imani ya ukafiri na shirki.

Ensaiklopidia ya kitabu cha dunia inaelezea mwaka mpya kwa maneno yafuatayo:

“Mtawala wa Kirumi, Julius Caesar, alianzisha Januari 1 kama Siku ya mwaka mpya katika 46 B.K .Warumi wakajitolea siku hii kwa Janus, mungu wa mageti, milango na mwanzo. January ilipewa jina la Janus, ambaye alikuwa na nyuso mbili-moja ikitazama mbele na nyingine ikitazama nyuma. Warumi wakwanza walipeana zawadi za mwaka mpya za matawi kutoka kwa miti mitakatifu. Baadaye walikuwa wakitoa sarafu zilizochorwa picha za Janus, au karanga zilizofunikwa kwa dhahabu.

Kutokana na ufafanuzi uliotajwa hapo juu, tunaelewa kuwa Siku ya mwaka mpya ni sherehe ya makafiri ambayo ina maana ya kidini. kwa hivyo haijuzu kwa Muumini kushiriki katika sherehe hii wala kuwa na uhusiano wowote nayo. vile vile haijuzu kwake kutakiana vizuri au kusema “heri ya mwaka mpya” kwao kwenye hafla hii. Allah Ta’ala anawaamrisha waumini katika Qur-aan tukufu:

وَلَا تَرکَنُوْا اِلَی الَّذِيْنَ ظَلَمُوْا فَتَمَسَّکُمُ النَّارُ

“Wala msiwaelekee wale waliojidhulumu nafsi zao (kwa kufanya shirki (kuabudu masanamu)) la sivyo mtapatwa na moto wa Jahannam”. (Surah hud aya ya 113)

Aya hii kwa uwazi kabisa inawakataza waumini kutokana na aina yoyote ya “mwelekeo kuelekea makafiri”. Maulamaa na Wanazuoni wanaeleza kwamba “kuelekea kwa makafiri” inahusu mtu anayeelekea kwenye imani, desturi, ibada, sherehe, mavazi na utamaduni wao. Kwa hiyo ushiriki wa namna hii kusherehekea, kutoa zawadi au kuwatakia watu “heri ya mwaka mpya” kwa hakika ni “mwelekeo wa makafiri” na hivyo kuwa hairuhusiwi.

Mbali na hayo, katika mikusanyiko ya mkesha wa mwaka mpya mziki hupigwa, pombe huliwa, wanaume na wanawake wanavaa bila heshima na kuchangamana kwa uhuru. Mazingira ni maovu na dhambi na yamejaa haramu na shughuli zisizo na haya.

Rasulullah (sallallaahu alaihi wasallam) amekataza mtu kushiriki katika mkusanyiko ambao watu wanahusika katika madhambi. kupitia kwa watu kushiriki katika mkusanyiko huo, mtu atakuwa akiunga mkono na madhambi kwa kuongeza idadi ya watu katika mkusanyiko.

Rasulullah (sallallaahu alaihi wasallam) alisema:

من كثر سواد قوم فهو منهم ومن رضي عمل قوم كان شريكا في عملهم

Atakaye ongeza idadi ya watu, basi atahesabiwa miongoni mwao (yaani mbele ya Allah Ta’ala) na mwenye kuridhia kosa ya watu basi atakuwa mshirika katika vitendo vyao.”

kwa hivyo kushiriki katika sherehe kama hiyo – iwe kwa bidii au kwa utulivu – ni hatari sana kwa imaan ya mtu. Kama waumini tunapaswa kuwa watiifu kwa Allah Ta’ala na kuilinda imaan yetu kwa kujiepusha kabisa na mambo yote yanayohusishwa na makafiri, sherehe zao na desturi zao. Kwa hivyo hatupaswi hata kuwa watazamaji wa sherehe zao na fataki, kwani hii pia ni aina ya ushiriki wa kimya.

Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo watu wanawaiga makafiri katika kuunga mkono sherehe ya mwaka mpya ya makafiri:

a. Kutangaza mauzo ya “mwaka mpya”.

b. Kutoa zawadi au kadi za “mwaka mpya” kwa wateja, wafanyakazi nk.

c. Kukaa macho hadi usiku wa manane kwenye 31 Desemba “kuona katika mwaka mpya”.

d. Kuchoma fataki usiku wa manane

Kama waumini tunaamini kwamba heshima ya kweli inaweza kupatikana tu kwa kufuata mafundisho safi ya Uislamu na sunna mubaraka ya Rasulullah (sallallaahu alaihi wasallam). Ikiwa tutatafuta heshima mahali pengine, hatutaleta chochote ila fedheha na unyonge kwetu wenyewe. Umar (radhiallahu anhu) amesisitiza:

إنا كنا أذل قوم فأعزنا الله بالإسلام فمهما نطلب العز بغير ما أعزنا الله به أذلنا الله

“Tulikuwa watu wenye kufedheheshwa zaidi kuliko watu wote. Allah Ta’ala kisha akatupa utukufu kwa njia ya Uislamu, ikiwa tutatafuta heshima katika kitu kisichokuwa kile ambacho Allah Ta’ala ametufariji nacho (Uislamu), basi Allah Ta’ala atatufehedhesha.

Na Allah Ta’ala ndiye Mjuzi zaidi.

About admin