عن عبد الملك بن سعيد بن سويد قال سمعت أبا حميد أو أبا أسيد الأنصارى يقول قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا دخل أحدكم المسجد فليسلم على النبى صلى الله عليه وسلم ثم ليقل اللهم افتح لى أبواب رحمتك فإذا خرج فليقل اللهم إنى أسألك من فضلك. (أبو داود الرقم: 465)
Abu Humaid au Abu Usaid (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Kila mtu anapoingia msikitini, kinabidi mtu atume salaam juu ya Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na kisha asome dua ifuatayo:
اللَّهُمَّ افْتَحْ لَنَا أَبْوَابَ رَحْمَتِك
Ewe Allah, nifungulie milango ya rehema zako.
Na anapotoka msikitini kinabidi atume salaam Kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na kisha asome dua ifuatayo:
اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ
Ewe Allah, nakuomba fadhila Zako.”
Kupata Msamaha kupitia Kuandika salaa na salaam
Ibnu Abi Sulaimaan (rahimahullah) anataja:
Nilimwona baba yangu katika ndoto baada ya kifo chake. Nilimuuliza, “jinsi gani Allah subhaana wata’ala Alikushughulikia?” Akajibu: “Allah subhaana wata’ala amenisamehe.” Nikauliza, “Ni kwa kitendo gani alichokusamehe?” Yeye
akajibu, “Nilikuwa nikiandika salaa na salaam baada ya jina la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika kila hadith.”