Bahili wa kweli

عن حسين بن علي بن أبي طالب قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: البخيل الذي من ذكرت عنده فلم يصل علي (سنن الترمذي، الرقم: 3546، وقال هذا حديث حسن صحيح غريب)

Sayyidina Husain (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “bakhili wa kweli ni yule ambaye jina langu linatajwa mbele yake, lakini hanitumii salamu.”

Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Akijibu Salamu

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Kila mtu anaponisalimia kwenye kaburi langu, Allah Ta’ala anarudisha rooh yangu kwenye mwili wangu ili nimjibu salamu yake.”

Katika Sharh-e-Manaasik, Haafidh Ibnu Hajar (rahimahullah) anaandika kwamba maana ya kurejea rooh ni kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) anampa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) uwezo wa kuzungumza. Qaadhi Iyaadh (rahimahullah) anaandika kwamba rooh ya Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) inabakia mbele ya Allah Ta’ala, na inaposalimiwa, basi inaelekea kwenye salamu.sw

Wengi wa Maulamaa (kama vile Haafidh Ibnu Hajar (rahimahullah) na ́Allaamah Zurqaani (rahimahullah) wana maoni kwamba maana ya kurejea kwa rooh sio kwamba mwili wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ulikuwa hauna rooh, alafu sasa umepewa rooh. Sababu ni kwamba rooh ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ilikuwa imerudishwa kwenye mwili wake baada ya kufariki kwake. Kwa hivyo, maana ya Hadith hii ni Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) anarejesha salamu.

About admin

Check Also

Kupokea Cheti cha Uhuru kutokana na Unafiki na moto wa Jahannam

عن أنس بن مالك قال: قال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم: من صلى …