عن أنس بن مالك قال: قال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم: من صلى علي صلاة واحدة صلى الله عليه عشرا ومن صلى علي عشرا صلى الله عليه مائة ومن صلى علي مائة كتب الله له بين عينيه براءة من النفاق وبراءة من النار وأسكنه الله يوم القيامة مع الشهداء (المعجم الصغير للطبراني، الرقم: ٨٩٩، وقال الهيثمي في مجمع الزوائد (الرقم: ١٨٢٩٨): رواه الطبراني في الصغير والأوسط وفيه إبراهيم بن سالم بن شبل الهجيمي ولم أعرفه وبقية رجاله ثقات، وقال المنذري في الترغيب والترهيب (الرقم: ٢٥٦٠): وفي إسناده إبراهيم بن سالم بن شبل الهجعي لا أعرفه بجرح ولا عدالة)
Anas (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, “yoyote atakae nitumia salaam mara moja, kwa kumlipa Allah subhaana wata’alah atamtumia salamu mara kumi (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara kumi, Allah subhaana wata’alah atamtumia salaam mara mia (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara mia, Allah subhaana wata’alah Atamwandikia (cheti) uhuru, katikati ya macho yake mawili, kutokana na unafiki, (na cheti ya) uhuru kutokana na moto wa jahannum, na Allah subhaana wata’alah ataampa heshma na faraja ya kuwa na mashahidi siku ya qiyamah.”
Kuwa Jirani wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Siku ya Qiyaamah
Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam ) amesema: “Mwenye kufunga safari makhsusi ya kuzuru kaburi langu atakuwa jirani wangu siku ya Qiyaamah, na mwenye kuishi Madinah Munawwarah na akavumilia shida na tabu zake, kwake mimi nitakuwa shahidi na muombezi siku ya Qiyaamah, na yule anayefariki mmoja katika Haramain (yaani Makkah Mukarramah au Madinah Munawwarah) atafufuliwa siku ya Qiyaamah pamoja na wale waliopewa usalama.”