Kila kipengele cha dini ya Kiislamu kinachohusiana na wanawake vimeengemezwa na unyenyekevu na aibu. Ni katika suala hili ndipo Uislamu unawaamrisha wanawake kubaki ndani ya mipaka ya nyumba zao, wakiwa wamejificha kabisa machoni kwa wanaume, na wasitoke majumbani mwao bila ya haja halali ya Sharia.
Namna ambayo mwanamke ameamrishwa kuswali – kuanzia kwenye vazi lake la Swalah hadi kwenye misimamo yake wakati wa Swalah – yote yanaelekeza kwa uwazi kwenye kipengele cha kujificha.
Hivyo basi, achilia mbali ibaadah zingine mbalimbali za Dini, Swalaah ya mwanamke peke yake inaonyesha kiwango kikubwa cha staha na aibu mwanamke anahitajika kuonyesha. Kwa hivyo, ameamrishwa kuchukua kiwango kile kile cha staha na aibu anayoonyesha kwenye Swalah yake katika idara zingine za Dini yake na maisha ya dunia.
Kujistiri
Ni ukweli usiopingika kwamba muundo wa kimwili wa wanawake ni tofauti na wanaume. Shari’ah imezingatia hili na hivyo ikaweka hukumu tofauti kwa wanaume na wanawake katika mambo mengi muhimu ya Deen.
Sababu ya msingi katika hukumu tofauti kwa wanawake ni kwamba wameamrishwa kufanya kila kitu kwa namna ambayo ni siri zaidi kwao. Tofauti hii pia imekuwa kuzingatiwa katika mikao mbalimbali ya Swalaah. Mwanamke ameamrishwa kutekeleza mikao yake kwa njia isiyo dhihirisha na kuficha zaidi.
Imaam Baihaqi ametaja:
وجماع ما يفارق المرأة فيه الرجل من أحكام الصلاة راجع إلى الستر وهو أنها مأمورة بكل ما كان أستر لها (السنن الكبرى للبيهقي، الرقم: 3196)
Vipengele vyote mbalimbali katika Swalaah ya mwanamke ambavyo vinatofautiana na Swalaah ya mwanamume (yaani namna ya kutimiza mikao mbalimbali ya Swalaah) vyote vimeegemezwa kwenye satr (kuficha). Mwanamke ameamrishwa kutekeleza kila jambo katika mikao wa swalah yake kwa namna ya kuficha umbo la mwili wake na viungo zaidi.
Sayyidina Abdullah bin Umar (radhiyallahu ‘anhu) Anasema kwamba katika zama za Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), wakati wa kuswali, wanawake waliamrishwa kuweka viungo vyao pamoja karibu iwezekanavyo.[1]
Madhehebu Nne
Tangu zama za Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum), Taabi’een (rahimahumallah) na karne zilizofuata, wanawake waliamrishwa kuswali kwa namna ambayo inatofautiana na swala ya wanaume katika vipengele fulani. Madhehebu nne hizi (yaani Hanafi, Maaliki, Shaafi’ee na Hambali) zote zinakubaliana kwamba Swalaah ya wanawake inatofautiana na Swalah ya wanaume katika nyanja fulani.[2]
[1] عن نافع عن ابن عمر رضي الله عنهما أنه سئل كيف كن النساء يصلين على عهد رسول الله صلى الله عليه وسلم كن يتربعن ثم أمرن أن يحتفزن (مسند الإمام الأعظم للحصكفي على ترتيب السندي صـ 73)
(عن نافع عن ابن عمر أنه سئل كيف كن النساء يصلين على عهد رسول الله صلى الله عليه وسلم) أي في زمانه صلى الله عليه وسلم (قال كن يتربعن) أي في حال قعودهن (ثم أمرن أن يحتفزن) بالحاء المهملة والفاء والزاء أي يضممن أعضاءهن بأن يتوركن في جلوسهن (شرح مسند الإمام أبي حنيفة للقاري صـ 191)
صححه العلامة ظفر أحمد العثماني في إعلاء السنن (3/27)
[2] المذهب الحنفي: ويجافي بطنه عن فخذيه كذا في الهداية والمرأة لا تجافي في ركوعها وسجودها وتقعد على رجليها وفي السجدة تفترش بطنها على فخذيها كذا في الخلاصة (الفتاوى الهندية 1/75)
المذهب المالكي: المرأة يندب كونها منضمة في ركوعها وسجودها (حاشية الدسوقي 1/249)
المذهب الشافعي: ولا فرق بين الرجال والنساء في عمل الصلاة إلا أن المرأة يستحب لها أن تضم بعضها إلى بعض وأن تلصق بطنها بفخذيها في السجود كأستر ما يكون وأحب ذلك لها في الركوع وفي جميع الصلاة وأن تكثف جلبابها وتجافيه راكعة وساجدة لئلا تصفها ثيابها وأن تخفض صوتها وان نابها شئ في صلاتها صفقت (المجموع شرح المهذب 3/346)
المذهب الحنبلي: تجمع نفسها في الركوع والسجود وسائر صلاتها (المغني لابن قدامة 1/339)