Mteremko Katika Ummah Kabla Dajjaal Kufika

Imetajwa katika Hadith kwamba kabla ya Qiyaamah, lengo la msingi la watu litakuwa kukusanya mali na fedha. Watu wataona utajiri kama ufunguo wa anasa zote na faraja, mlango wa kila aina ya burudani, na chombo cha kutimiza raha zao za kidunia na tamaa za kidunia. Kwa hivyo, watatoa kila kitu kuipata na watafanya chochote kuipata.

Shauku kubwa ya mali itawatuma na kuwafanya kutokujali kabisa na kutokuwa na wasiwasi kwenye majukumu yao ya Dini. Katika harakati za kutafuta mali, watakuwa watu wasiofaa katika shughuli zao na kuathiri maadili yao ya dini. Hata kama wanalazimishwa kupinga au kuvunja sheria za dini ili kupata mali zaidi, hawatasita kufanya hivyo.

Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Hivi karibuni wakati utafika kwa watu ambao hawatojali jinsi gani wanapata mali zao, iwe ni kutoka kwa vyanzo vya Halaal au Haraam.” (Saheeh Bukhaari #2059)

Imeripotiwa katika Hadith moja kwamba kabla ya Qiyaamah, kwa sababu ya ubinafsi na watu kupenda mali, watu watakuwa tayari kuuza dini yao kupata kitu fulani cha kidunia.

Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “harakisheni katika vitendo meema kabla ya fitnah kuanza ambayo itakuwa kama sehemu ya usiku wa giza. Mtu atakuwa mwamini asubuhi na kuwa kafiri jioni, au mtu atakuwa mwamini jioni na kuwa kafiri asubuhi. Atakuwa tayari kuuza Deen yake kwa milki ya dunia. ” (Saheeh Muslim #118)

Ikiwa mtu atachunguza fitna za wakati huu ndani ya waislamu na changamoto mbali mbali zinazowakabili Ummah, utagundua kuwa wanapitia changamoto zilizoelezewa katika hadithi hii aliyetajwa hapo juu. Imeripotiwa katika Hadith kwamba wakati Dajjaal atatokea, atatumia zana hii ya mali kupotosha watu.

About admin

Check Also

Dalili Za Qiyaamah Part 4

Dalili Kumi Kubwa Za Qiyamah Kama jinsi kuna dalili nyingi ndogo za Qiyaamah zilizorekodiwa katika …