Vifaa za Dajjaal – Utajiri, Wanawake na Burudani

Wakati Dajjaal ataonekana ulimwenguni, vitu ambazo atatumia kupotosha mwanadamu zitakuwa utajiri, wanawake na burudani.  Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) atampa nguvu ya kutekeleza mambo yasio ya kawaida hadi kwamba wote wanaoshuhudia watashawishiwa na kutapeliwa na wimbi la Fitnah yake.

Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) atamruhusu kusababisha mawingu kunyesha, kufanya ardhi itoe mazao na utajiri wa dunia utamfuata popote aendako. Utajiri wa dunia utamfuata kama vile ameer wa nyuki wanamfuata na kundi lake la nyuki. Kwa hivyo, njaa na uchoyo ambao watu wanayo kwa kupata utajiri itawaendesha kumfuata Dajjaal, baada ya hapo watafuata njia zake za udanganyifu na kujiunga na safu zake, na hivyo kupoteza Imaan.

Akielezea ukali wa Fitnah za Dajjaal, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema:

“… Dajjaal atakuja kwa watu na kuwaalika (kumkubali kama Mwenyezi Mungu). Wataleta Imaan kwake na watakubali mwaliko wake. Kwa hivyo ataamuru anga na itanyesha, na atamuru dunia na itazalisha mazao. Kwa hivyo, mifugo yao itarudi kwao jioni na vibanda vyao virefu kuliko vile waliondoka nayo, mazwa yao yakijaa kuliko vile yalikuwa, na miguu yao kunenepa kuliko vile yaliwahi kuwa. Dajjaal basi atakwenda kwa watu wengine na kuwaalika (kuamini kuwa yeye ni Mwenyezi Mungu). Lakini, watakataa mwaliko wake. Kwa hivyo atawaacha, na baadaye watakuwa katika hali ya ukame na hawatakuwa na utajiri wao tena. Dajjaal atapita hio sehemu iliyoharibika na atasema, “Toa hazina zako!” Kwa hivyo, hazina hizo zitamfuata kama Malkia wa nyuki anafuatwa na nyuki zake… ”(Saheeh Muslim #2937)

Katika Hadith moja, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alielezea kwamba wafuasi wakuu wa Dajjaal watakuwa Wayahudi, wanawake na wale ambao wanahusika katika faida na riba. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Wafuasi wake wengi (Dajjaal) watakuwa Wayahudi na wanawake (wanawake wasio na dini).” (Majma’uz Zawaa’id #12520)

Katika simulizi moja, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Wafuasi wake wengi (yaani Dajjaal) na mawakala siku hiyo (wakati Dajjaal anaibuka) watakuwa watu wanaohusika na riba.” (Fitan Lid-Daani #665)

Jinsi muda unavyozidi kupita, hali ya Dini katika Ummah ulimwenguni inazidi kudhoofika na mfumo wa thamani wa watu waulaya unawazidi. Kama matokeo, upendo wa utajiri na tamaa ya vitu vya kidunia hushuhudiwa kila mahali. Maisha ya watu wengi yanazingatia burudani na kufurahishwa.

Miaka iliyopita, watu wa ulaya waligundua kiwango cha hamu ya mwanadamu anayo kwenye burudani na wakamua kuitumia kuwapoteza watu. Kwa hivyo, waligundua hamu ya mwanadamu kwenye burudani na walianza ‘tasnia za burudani’ ambayo sasa inaonekana kuwa inakua na kustawi ulimwenguni. Kiwango cha haraka ambacho tasnia za burudani za bilioni zakidola ‘imeendelea na inaendelea kustawi ni dhibitisho la hamu ya mwanadamu katika mambo za kufurahisha na burudani.

Kwa kuongeza, uvumbuzi wa TV, kompyuta na simu za kisasa imeongeza tu hamu ya mwanadamu ya burudani na kiu chake cha kufurahishwa. Kwa hivyo, wakati Dajjaal ataibuka, atawapotosha watu wanaotumia zana hizi za burudani, wanawake na mali, ambazo ni sehemu dhaifu kwa mwanadamu.

Wakati mtu anatafakari juu ya suala hilo, ni wazi kuwa ‘kuishi kwa burudani’ ni thamani ya msingi ya mawazo ya makafiri. Sababu ya hii ni kwamba makafiri hawana wazo na imani ya Aakhirah na kwa hivyo wanaishi kwa hii dunia na wankufa kwa hii dunia. Wanaona dunia hii kama ‘kila kitu kwao’. Wakati wanachukuwa dunia hii kuwa Jannah yao, wanafanya bidii ya kubadilisha kila wakati kuwa yakistarehe na burudisho.

Ndani ya Qur’ani, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) anaelezea maisha ya Kaafiri kuwa ya kula na starehe. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) anasema, “Wale ambao wanamkataa Mwenyezi Mungu hufurahiya (dunia hii) na kula kama wanyama wanavyokula; na moto (wa Jahannum) itakuwa makazi yao.” (Surah Muhammad aya 12)

Wakati Kafiri hana wazo na imani ya Aakhirah, Jannah na Jahannum, na kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) kwa kufikiria, basi inatarajiwa kwake kuwa na fikra kama hizi juu ya burudani. Lakini, hii haitarajiwi kwa mumini.

Mumini na kafiri ni kama miti miwili mbali mbali katika imani zao na akili. Kusudi na lengo la mumini ni kujitahidi kumfurahisha Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) na malengo ya juu ya Aakhirah. Kwa hivyo, anajaribu kutumia kila wakati duniani kujiandaa kwa makazi yake ya milele huko Akhera.

Kwa hivyo, watu ambao watalindwa na Fitnah ya Dajjaal watakuwa wale ambao hawajihusishi na starehe na burudani ya ulimwengu huu kuwa lengo lao lakini badala yake watawekeza kwa ajili ya Aakherah. Kwa wale ambao wanafuata ulimwengu huu kila wakati na kuifanya iwe lengo lao la msingi, watakuwa wafuasi wakuu wa Dajjaal.

About admin

Check Also

Dalili Za Qiyaamah Part 4

Dalili Kumi Kubwa Za Qiyamah Kama jinsi kuna dalili nyingi ndogo za Qiyaamah zilizorekodiwa katika …