Uadilifu na Baraka Wakati wa Utawala wa Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Utawala wa Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) utakuwa wa uadilifu na wa baraka. Kwa kuwa Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) amechaguliwa na Allah Ta‘ala kuongoza ummah kabla ya Qiyaamah, basi ataongozwa na Allah Ta‘ala. Kwa hiyo, kila uamuzi atakaoupitisha utajawa na wema na uadilifu. Wakati wa utawala wake, Allah Ta’ala atawabariki Waislamu kwa baraka nyingi na atarejesha nguvu na heshima ya Uislamu katika ummah.

Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) atatokea katika zama za mwisho wa Ummah wangu, Allah Ta‘ala atamjaalia baraka nyingi kwa kusababisha mvua kubwa inyeshe kutoka mbinguni, ambayo ardhi itatoa mazao mengi. Atagawa mali kwa uadilifu baina ya Waislamu, mifugo itaongezeka na kupatikana kwa wingi na ummah kwa mara nyingine tena utapata nguvu na heshima yake. Baada ya kuteuliwa na Allah Ta’ala, ataishi miaka saba au minane.” (Mustadrak Haakim #8673)

About admin

Check Also

Vifaa za Dajjaal – Utajiri, Wanawake na Burudani

Wakati Dajjaal ataonekana ulimwenguni, vitu ambazo atatumia kupotosha mwanadamu zitakuwa utajiri, wanawake na burudani.  Mwenyezi …