Monthly Archives: July 2021

Kupata Maombezi Ya Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن رويفع بن ثابت قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى على محمد وقال: اللهم أنزله المقعد المقرب عندك يوم القيامة، وجبت له شفاعتي (المعجم الكبير للطبراني، الرقم: ٤٤٨٠، وإسناده حسن كما في مجمع الزوائد، الرقم: ١٧٣٠٤) Sayyidina Ruwaifi Bin Thaabit Al ansaari (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba …

Soma Zaidi »

Kutokomeza Kwa Umasikini

Sayyidina Samurah Suwaai (radhiallahu anhu), baba wa Sayyidina Jaabir (radhiallahu anhu), ameripoti kwamba: tuliwahi kuwa na Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) pindi mtu mmoja alikuja kwa Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na akauliza, " ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) !ni tendo gani linalomrizisha Allah subhaana wata'alah zaidi?" Nabii wa Allah-(sallallahu alaihi wasallam) akajibu, "maneno ya ukweli na kutimiza uwaminifu." Nikasema, "ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Nakuomba utuzidishie nasaha (kuhusu matendo yanayo mrizisha Allah subhaana wata'alah)!" Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, " swali wakati wa usiku na funga wakati wa jua kali." Kisha nikasema, ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Nakuomba utuzidishie nasaha!" Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, " jishughulishe na zikr kwa wingi na nitumie salaam inaondowa umasikini," nikauliza tena, ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) nakuomba utuzidishie nasaha! Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, yule atakae  swalisha  watu basi  afupishe swala,kwa sababu kwenye jamaa  kuna wazee, kuna wagonjwa, vijana na watu kuna ambao wana dharura."

Soma Zaidi »

Kukubalika Kwa Dua

Imepokelewa kutoka kwa Umar (radhiallahu anhu) dua zinabaki zimesimamishwa kati ya mbigu na ardhi. Hazitafika mbinguni Kama salaam haijatumwa kwa Nabii (sallallahu alaihi wasallam) (yaani hakuna uwakika wa kukubalika)."

Soma Zaidi »

Ongezeko la rizki

Sahl bin Sa'd (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba kuna wakati mmoja, sahaba mmoja alimfata Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Na akalalamika juu ya umasikini na ugumu wa kupata rizki. Nabi wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akamuambia huyu sahaba, "pindi unapo ingia nyumbani kwako, kuwepo watu ndani au hata kama hamna watu ndani basi toa salaam. Baada ya hapo nitumie mimi salaam na soma Qul-Huwallah (surah ikhlaas) mara moja". Sahaba akafanya jinsi alivyo amrishwa na Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam), na Allah subhaana wata'alah akambariki kwa utajiri mwingi na akaanza kutumia kwa majirani na ndugu zake.

Soma Zaidi »