Ongezeko la rizki

عن سهل بن سعد رضي الله عنه قال: جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه وسلم فشكا إليه الفقر وضيق العيش أو المعاش فقال له رسول الله صلى الله عليه وسلم: إذا دخلت منزلك فسلم إن كان فيه أحد أو لم يكن فيه أحد ثم سلم علي واقرأ قل هو الله أحد مرة واحدة ففعل الرجل فأدَرَّ الله عليه الرزق حتى أفاض على جيرانه وقراباته (أبو موسى المديني وسنده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٧٩)

Sahl bin Sa’d (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba kuna wakati mmoja, sahaba mmoja alimfata Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Na akalalamika juu ya umasikini na ugumu wa kupata rizki. Nabi wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akamuambia huyu sahaba, “pindi unapo ingia nyumbani kwako, kuwepo watu ndani au hata kama hamna watu ndani basi toa salaam. Baada ya hapo nitumie mimi salaam na soma Qul-Huwallah (surah ikhlaas) mara moja”. Sahaba akafanya jinsi alivyo amrishwa na Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam), na Allah subhaana wata’alah akambariki kwa utajiri mwingi na akaanza kutumia kwa majirani na ndugu zake.

Jina la Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) ndani ya Taurah

Allaamah Sakhawi (rahimahullah) anaeleza:

Kuliwahi kuwa mtu mbaya kati ya Bani Israeel. Wakati alipofariki, watu hawa kuumpa heshma yoyote na wakaucha mwili wake chini. Allah Ta’laa alimshushia wahyi moosa (alaihis salaam), “ewe moosa (alaihis salaam), muoshe na umsaliye sala ya janaza, kwa sababu tayari nimemsamehe madhambi zake”.

Moosa (alaihis salaam) akauliza, “ewe Allah subhaanawata’alah, sababu ya hili ni nini?” Allah Ta’la Akamjibu, “wakati mmoja macho yake yaliangukiya kwenye jina la Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) ndani ya Taurah na akamtumia salaam Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Kupitia hili tendo, nimemsamehe”.  (Al Qawlul Badee, Pg, 260)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …