Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl- Sehemu Ya Nne

13. Mimina maji mwilini upande wakulia kutoka juu ya mwili mpaka chini mara tatu, baada ya hapo mimina maji mwilini upande wa kushoto kutoka juu ya mwili mpaka chini mara tatu. Sunnah itakua imetimizwa kwa kuosha mwili kwa njia hii. Pia ni sahihi kuosha upande wa kulia mara moja , kufuata upande wa kushoto mara moja, na kurudia hii njia kwa mara ya pili na ya tatu. Sunna itakuwa imetimizwa kwa njia hii pia. Pindi unapo mimina maji mwilini, mimina maji mbele ya mwili kabla ya nyuma.[1]

14. Hakikisha maji yanafika sehemu zote mwilini. Kila mara ukimimina maji mwilini, suguwa mwili kuhakikisha maji yanafika kwenye ngozi. Kama sehemu yoyote pameachwa pakavu sawa sawa na upana wa nywele, basi ghusl ya fardh itakua haijakamilika. Pindi unapo osha mwili, anza mbele kabla ya nyuma.[2]

عن علي رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال من ترك موضع شعرة من جنابة لم يغسلها فعل بها كذا وكذا من النار قال علي فمن ثم عاديت رأسي ثلاثا وكان يجز شعره (سنن أبي داود، الرقم: ٢٤٩)[3]

Sayyidina Ali (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Amesema, “yoyote ambae yuko ndani ya janaba (anahitaji ghusl ya fardh) na anaacha sehemu (mwilini) sawa sawa na upana wa nywele bila kuoshwa, basi ile sehemu itaadhibiwa ndani ya jahannam”. Kisha Sayyidina Ali (radhiyallahu ‘anhu) akasema mara tatu, “ndo mana sipendi kufuga nywele”. Imeripotiwa kwamba Sayyidina Ali (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ananyowa nywele zake (kwa kuogopa kwamba pindi anapo fanya ghusl, hamna nywele itaachwa pakavu na kusababisha ghusl kuwa haijakamilika).

15. Usiharibu maji pindi unapo fanya ghusl. Maji mengi sana yasitumiwe na maji madogo sana ambayo mtu hawezi kuosha mwili vizuri pia yasitumiwe.

عن عبد الله بن محمد بن عقيل بن أبي طالب عن أبيه عن جده رضي الله عنهم قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم يجزئ من الوضوء مد ومن الغسل صاع فقال رجل لا يجزئنا فقال قد كان يجزئ من هو خير منك وأكثر شعرا يعني النبي صلى الله عليه وسلم (سنن ابن ماجة، الرقم: ٢٧٠)[4]

Sayyidina Aqeel Bin Abi Taalib (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Amesema, “Mudd moja ya maji inatosha kufanya udhu, na Saa’ moja ya maji inatosha kufanya ghusl”. Mtu mmoja aliskia hili na akasema, ” Hii idaadi ya maji haitatosheleza”. Sayyidina Aqeel (radhiyallahu ‘anhu) alimfokea na akamjibu, “ilimtosheleza mtu ambaye ni mbora kwako na alikuwa na nywele nyingi kukuzidi (anamaanisha Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam))”. (Mudd na Saa’ ni aina ya vipimo)


[1] يفيض الماء على رأسه ثم على شقه الأيمن ثم الأيسر ويكون غسل جميع البدن ثلاثا كالوضوء فإن اغتسل في نهر ونحوه انغمس ثلاث مرات ويدلك في كل مرة ما يصل يده (روضة الطالبين ١/٢٠٢)

(ويثلث) بالشروط السابقة في الوضوء تخليل رأسه ثم غسله للاتباع ثم تخليل شعور وجهه ثم غسله ثم تخليل شعور بقية البدن ثم غسله قياسا عليه

وهذا الترتيب ظاهر وإن لم أر من صرح به وتثليث البقية إما بأن يغسل شقه الأيمن ثم الأيسر ثم هكذا ثانية ثم ثالثة أو يوالي ثلاثة الأيمن ثم ثلاثة الأيسر وكان قياس كيفية التثليث في الوضوء تعين الثانية للسنة واقتضاه كلام الشارح لكن من المعلوم الفرق بين ما هنا وثم فإن كلا من المغسول ثم كاليدين متميز منفصل عن الآخر فتعينت فيه تلك الكيفية لذلك بخلاف ما هنا فإن كون البدن فيه كالعضو الواحد منع قياسه على الوضوء في خصوص ذلك وأوجب له حكما تميز به وهو حصول السنة بكل من الكيفيتين فتأمله (تحفة المحتاج ١/٢٩٧)

[2] يفيض الماء على (شقه الأيمن) مقدمه ثم مؤخره (ثم) بعد فراغه منه جميعه يفيضه على شقه (الأيسر) كذلك (تحفة المحتاج ١/٢٩٦)

[3] سكت الحافظ عن هذا الحديث في الفصل الثاني من هداية الرواة (١/٢٣٥) فالحديث حسن عنده

[4] قال البوصيري في الزوائد (١/٩٩): إسناده ضعيف لضعف حبان ويزيد

لهذا الحديث شاهد من حديث ابن عباس قال قال رجل كم يكفيني للوضوء قال مد قال كم يكفيني للغسل قال صاع قال فقال الرجل لا يكفيني فقال لا أم لك قد كفى من هو خير منك رسول الله صلى الله عليه وسلم رواه أحمد والبزار والطبراني في الكبير ورجاله ثقات (مجمع الزوائد الرقم: ١٠٩٩)

About admin

Check Also

Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl- Sehemu Ya Tano

16.usijeshughulishe na kuongea, au kuimba au mazungumzo yoyote pindi utakapokuwa unafanya ghusl.

17. Usitumiye muda mwingi bafuni haswa kama bafu yenyewe inatumiwa na watu wengine.

18. Usichafuwe bafu na nywele ulizo nyowa.