Dua Na Adhkaar Kabla Ya Kulala 2

Dua ya Tano

بِاسْمِكَ رَبِّ وَضَعْتُ جَنْبِيْ وَبِكَ أَرْفَعُهُ إِنْ أَمْسَكْتَ نَفْسِيْ فَارْحَمْهَا وَإِنْ أَرْسَلْتَهَا فَاحْفَظْهَا بِمَا تَحْفَظُ بَهِ عِبَادَكَ الصَّالِحِيْنَ

Kwa jina Lako, ewe mola wangu, naweka ubavu wangu (kitandani), na kwako (yaani kwa jina lako na usaidizi) ninauinua (wakati wa kuamka). Ukiichukua nafsi yangu (katika usingizi wangu) basi irehemu, na ukiiacha (yaani kuniruhusu niamke nikiwa hai) basi uilinde (kwa kutokutenda madhambi) kwa (kinga maalum na tawfeeq) ambayo unawalinda waja Wako wema.

Dua ya Sita

اَللّٰهُمَّ خَلَقْتَ نَفْسِيْ وَأَنْتَ تَوَفَّاهَا لَكَ مَمَاتُهَا وَمَحْيَاهَا إِنْ أَحْيَيْتَهَا فَاحْفَظْهَا وَإِنْ أَمَتَّهَا فَاغْفِرْ لَهَا اَللّٰهُمَّ إِنِّيْ أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةْ

Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah)! Umeiumba nafsi yangu, na utaichukua. Kwa sababu yako pekee inakufa na kuishi. Ukiiacha hai (baada ya kulala) basi ilinde (kwa kuto kutenda madhambi), na ukiifisha basi isamehe. Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah)! Ninakuomba Aafiyah (starehe na wepesi).

Dua ya Saba

اَللّٰهُمَّ رَبَّ السَّمَاوَاتِ وَرَبَّ الْأَرْضِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيْمِ رَبَّنَا وَرَبَّ كُلِّ شَيْءٍ فَالِقَ الْحَبِّ وَالنَّوٰى وَمُنْزِلَ التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيْلِ وَالْفُرْقَانِ أَعُوْذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ شَيْءٍ أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ اَللّٰهُمَّ أَنْتَ الْأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شَيْءٌ وَأَنْتَ الْآخِرُ فَلَيْسَ بَعْدَكَ شَيْءٌ وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَيْءٌ وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُوْنَكَ شَيْءٌ اِقْضِ عَنَّا الدَّيْنَ وَأَغْنِنَا مِنَ الْفَقْرِ

Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah)! Mola wa mbingu, Mola wa ardhi, Mola wa enzi tukufu, Mola wetu na Mola wa kila kitu! Yule ambaye hupasua nafaka na mbegu, na aliye teremsha  Tawrah, Injili na Furqaan (Qur’an Majeed). Najikinga Kwako kutokana na shari ya kila kitu unachokishika na kisogo. Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah)! Wewe ndiye wa Kwanza, kwa hivyo hapakuwa na kitu kabla Yako, na Wewe ndiyo wa mwisho, kwa hivyo hakutakuwa na kitu baada Yako, na Wewe ndiyo Mwenye Dhahiri (kupitia ishara Zako), kwa hivyo hakuna kitu juu Yako (kwa kudhihirika), na Wewe ndiye uliyefichika zaidi, kwa hivyo hakuna kitu chini yako (yaani hakuna kilichofichika zaidi yako wewe). Tukamilishie madeni yetu na ututajirishe kutoka kwa umasikini.

About admin

Check Also

Sunna na Aadaab Za Kulala 4

14. Ukiona ndoto nzuri, basi sema Alhamdulillah. Unaweza kumsimulia mtu ambaye ana ujuzi katika tabiri …