Dua za Sunnah Wakati wa Kuamka

Dua Ya Kwanza

اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ الَّذِيْ أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا وَإِلَيْهِ النُّشُوْرْ

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) aliyetujaalia maisha baada ya kufa na kwake Yeye tu tutarejeshwa.

Dua Ya Pili

اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ الَّذِيْ عَافَانِيْ فِيْ جَسَدِيْ وَرَدَّ عَلَيَّ رُوْحِيْ وَأَذِنَ لِيْ بِذِكْرِهِ

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) aliyenijaalia faraja ndani ya mwili wangu, na akanirudishia nafsi yangu, na akaniruhusu nimkumbuke.

Dua za Sunnah Wakati wa Kuamka Kuswali Tahajjud

Baada ya kuamka kwa ajili ya Tahajjud, soma aya kumi za mwisho za Sura
Aal Imraan. Pia soma yafuatayo kabla ya kuanza swalah ya Tahajjud:

(1) Allahu Akbar mara kumi

(2) Alhamdulillah mara kumi

(3) Subhanallahi wa bihamdihi mara kumi

(4) Subhaanal Malikil Quddoos mara kumi

(5) Astaghfirullah mara kumi

(6) Laa ilaaha illallah mara kumi

Baada ya hapo, soma dua ifuatayo mara kumi:

اَللّٰهُمَّ إِنِّيْ أَعُوْذُ بِكَ مِنْ ضِيْقِ الدُّنْيَا وَضِيْقِ يَوْمِ الْقِيَامَة

Ewe Mwenyezi Mungu! Natafuta ulinzi Wako kutokana na vikwazo vya dunia hii na vikwazo vya Siku ya Qiyaamah.

Katika riwaya ya Sunan Ibn Maajah, imepokewa kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) pia alisoma dua ifuatayo mara kumi:

اَللّٰهُمَّ اغْفِرْ لِيْ وَاهْدِنِيْ وَارْزُقْنِيْ وَعَافِنِيْ

Ewe Mwenyezi Mungu! Nisamehe, nibariki kwa kuniongoza, nijalie riziki na unijaalie Aafiyah (starehe na wepesi).

About admin

Check Also

Dua Na Adhkaar Kabla Ya Kulala 4

Dua Ya kumi لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ …