Katika mwaka wa 13 baada ya nubuwwah, watu 70 kutoka Answaar walikuja kuhijji na kusilimu mikononi wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Miongoni mwao alikuwa Muaaz bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye alikuwa katika kabila la Banu Salimah la Answaar, na alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo katika kabila lake kuukubali uisilimu.
Wakati Answaar waliporejea Madinah Munawwarah baada ya Hijja, walianza kuwalingania watu katika Uislamu. Wengi wa ukoo wa Banu Salimah walikuwa wamesilimu isipokuwa wachache wa wazee waliobakia kwenye ukafiri. Miongoni mwao alikuwa ni Amr bin Jamooh ambaye alikuwa miongoni mwa machifu na viongozi wa kabila la Banu Salimah kabla ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kuja Madinah Munawwarah.
Amr bin Jamooh alikuwa akiweka sanamu la mbao lililoitwa Manaat nyumbani kwake. Alikuwa akiliabudu sanamu hili na kulionesha heshima kubwa. Siku moja, vijana wachache wa kabila la Banu Salimah waliosilimu waliamua kulitupa sanamu la Amr bin Jamooh jalalani walipopata fursa ya kufanya hivyo. Kwa hiyo, usiku Muaz bin Amr (Radhiya Allaahu ‘anhu) – mtoto wa Amr bin Jamuuh ambaye alikuwa amesilimu, pamoja na Muaaz bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu), na kundi la vijana wengine, kwa siri waliingia ndani ya nyumba ya Amr bin Jamuuh, wakaliondoa sanamu lake juu na kulitupa chini kwenye sehemu moja ya taka taka la Banu Salimah ambapo watu walikuwa wakitupa uchafu wao.
Amr bin Jamooh alipoamka asubuhi na kukuta sanamu lake halipo, akasema: “laana iwe juu yako, ni nani aliyemdhulumu mungu wetu (kwa kuiba) usiku? Kisha akatoka kwenda kuitafuta, hadi mwishowe akaikuta ikiwa imelala chini kwenye jalala. Alipoipata, akaiokota, akaiosha, na kuipaka manukato, na akaiambia: “Wallahi, nikijua ni nani aliyekufanyia hivi, hakika nitamdhalilisha.
Kila usiku uliopita baada ya hapo, Amr bin Jamuuh alipokuwa akienda kulala, Muaaz bin Jabal na Muaz bin Amr (Radhiyallahu ‘anhuma), pamoja na kundi la vijana, walikuwa wakilifanya jambo hilo hilo kwa sanamu lake. Asubuhi iliyofuata, baada ya kuamka, Amr bin Jamooh angekuta sanamu lake halipo, na alikuwa akitoka tena kulitafuta. Alipoipata, aliiosha, na kuipaka manukato.
Hayo yalipoendelea kwa muda, Amr bin Jamooh alining’iniza upanga wake kwenye shingo ya sanamu hilo na kulihutubia akisema, “Wallahi sijui ni nani anayekufanyia hivi, lakini ikiwa kuna wema wowote ndani yako, basi utaweza kujilinda! Huu hapa upanga ninaokupa (ili kujilinda na waovu).”
Usiku huo, Muaz bin Jabal na Muaaz bin Amr (Radhiyallahu ‘anhuma), pamoja na kundi la vijana, walirudi tena kwenye nyumba ya Amr bin Jamuuh kuchukua sanamu lake. Wakautoa upanga shingoni mwa sanamu, wakamfunga mbwa uliokufa, wakatupa wote wawili – mbwa pamoja na sanamu imefungwa – katika moja ya visima vya kabila la Banu Salimah vilivyojaa takataka za watu na upotevu.
Asubuhi iliyofuata, Amr bin Jamooh kwa mara nyingine tena alilikuta sanamu lake halipo. Akatoka kuitafuta mpaka akaikuta kwenye jalala lililokuwa limefungwa na mbwa aliyekufa. Alipoiona katika hali la kufedhehesha, alitambua ukweli na akasilimu. Kisha akaliambia sanamu hilo akisema:
تالله لو كنت إلها لم تكن أنت وكلب وسط بئر في قرن
Wallahi! Ikiwa ungekuwa mungu, wewe na mbwa msingefungwa pamoja katikati ya kisima!
أف لمصرعك إلها مستدن الآن فتشناك عن سوء الغبن
Ole wako kama mungu aliyedharauliwa na hali uko kwenye uchafu na takataka! Sasa kwa kuwa tumekuchunguza kwa makini, tumekuona (yaani kukuabudu) kuwa ni mpango mbaya!
فالحمد لله العلي ذي المنن الواهب الرزاق وديان الدين
Basi sifa njema zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Aliye juu, Mwenye fadhila zote, Mwingi wa baraka zote, Mruzuku, na Aliyeituma Dini ya Haki (ya Uislamu).
هو الذي أنقذني من قبل أن أكون في ظلمة قبر مرتهن
Yeye ndiye aliyenipa uwokovu (kupitia Imaan) kabla sijanaswa katika giza la kaburi!
بأحمد المهدي النبي المرتهن
Aliniokoa kupitia Ahmed (Sallallahu alaihi wasallam), Nabii aliyeongoka ambaye ni msimamizi wa Dini ya Uislamu.
(Rowdhul Unuf 2/279)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu