Sunna Na Adabu Za Kufanya Istinja

Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Tano

17. Chukuwa tahadhari sana kuhakikisha kuwa hupatwi na cheche za mkojo mwilini. Hukifanya uzembe kwa hili kuna adhabu kaburini.

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) alisema kuwa mtume (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema ” adhabu kali (zitakazo wakabili watu wengi) kaburini ni adhabu za mkojo (mf: mtu kutokuwa makini kwa cheche za mkojo ambazo zinampata. Kwa ajili ya hilo udhu, sala zao na ibada zingine hazitokubalika kwa kuwa mtu anakuwa mchafu”)

Soma Zaidi »

Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Nne

11. Usizungumze ukiwa unajisaidia, labda kuwe na shida muhimu wa kuongea.

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu 'anhu) alitowa taarifa kuwa Nabii wa Allah subhaana wata'alah (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema "watu wawili wasiende pamoja kujisaidia sehemu moja na kuongea pamoja wakiwa watupu (yaani sehemu zao za siri) ziko wazi kwa hakika mwenyezi mungu hapendi kitendo hicho.

Soma Zaidi »

Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Tatu

7. Ingia chooni na mguu wako wa kushoto

8. Usivuwe nguo yako ukiwa umesimama anza kuvua nguo yako ukiwa umekaribia chini hili utumie muda mchache kwa kufunua sehemu zako za siri.

Sayyidina Abdullah Bin Umar (radhiyallahu 'anhuma) ametowa ripoti kuwa pindi Nabii wa Allah subhaana wata'alah (sallallahu 'alaihi wassallam) alipokuwa anataka kujisaidia alikuwa hapandishi nguo yake mpaka akaribie kufika chini.

Soma Zaidi »

Jinsi Ya Kujisaidia Na Kufanya Istinja (Istinja Ni Kutumia Maji Baada Ya Kujisaidia) – Sehemu Ya Kwanza

Umuhimu Wa Usafi Uislaam ni dini iliyokamilika na iliyo safi. Uislaam ni dini inayotufundisha usafi kwa njia zote za maisha ya mwanadamu. Nabii ﷺ amesema: الطهور شطر الإيمان “usafi ni nusu ya imani”[1] Ukweli ni kwamba, uislaam unatuongoza katika njia na kutuonesha jinsi ya kukaa kwenye usafi wa ndani na …

Soma Zaidi »