Jinsi Ya Kujisaidia Na Kufanya Istinja (Istinja Ni Kutumia Maji Baada Ya Kujisaidia) – Sehemu Ya Kwanza

Umuhimu Wa Usafi

Uislaam ni dini iliyokamilika na iliyo safi. Uislaam ni dini inayotufundisha usafi kwa njia zote za maisha ya mwanadamu. Nabii ﷺ amesema:

الطهور شطر الإيمان

“usafi ni nusu ya imani”[1]

Ukweli ni kwamba, uislaam unatuongoza katika njia na kutuonesha jinsi ya kukaa kwenye usafi wa ndani na nje. Kama tulivyo amrishwa kuwa wa safi kimwili na kinywa, pia tumeamrishwa kuwa wasafi kiroho na kulinda akili zetu kutokana na madhambi,m.f wivu, kibri, uchoyo, n.k.Allah subhaana wata’alah amesema katika qur an tukufu:

قَدْ افلح من تزكى

Hakika amefaulu atakaye itakasa nafsi yake[2]

Kama mtu atakuwa na mtazamo mbali mbali wa kufuata maamrisho ya kisheria m.f mtu kutawadha baada ya kutoka kujisaidia, kutawadha kwa ajili ya kuswali, kupiga mswaki baada ya kuamka, kabla ya swala, ikiwa kinywa kinatowa harufu mbaya, kabla ya kulala, nakadhalika, oga kabla ujaingia katika ihraam au kuingia kwenye majilisi siku ya eid au siku ya ijumaa, mtu atakuja kujuwa kuwa uislaam ni dini ambayo iko juu katika kusisitiza usafi wa hali ya juu kwa njia zote za maisha ya mwanadamu.

Nabii ﷺ amesema: “kuna matendo manne ya sunna kutoka kwa manabii wote عليهم السلام; nayo ni kuwa na haya(kuwa na aibu kwenye harakati zote za maisha ya mwanadamu), kama kupakaa atari, (pafyumu) kupiga miswaki, kufunga ndoa (kuoa)”[3]

Tukiangalia kwa makini matendo ambayo yametajwa kwenye hadith iliyopita, tutapata husiano wa kupata usafi wa ndani na nje.

Kwa upande mwingine kuna adhabu kali zilizotajwa kwenye hadith kwa ajili ya kukataa kufanya usafi. Ukiwa ghafiri kwa kujisafisha mwenyewe,utabaki mchafu, kwahiyo utakuwa amesababisha swala yako na ibada zingine zako ambazo usafi ndani mwake ni sharti kutokubalika. Kama vile kupuuzia usafi wa kinywa na mwili mtu atakuwa amesababisha usumbufu kwa watu wengine.


[1] عن أبي مالك الأشعري قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم الطهور شطر الإيمان (صحيح مسلم، الرقم: ٢٢٣)

[2] سورة الأعلى: ١٤

[3] عن أبي أيوب رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم أربع من سنن المرسلين الحياء والتعطر والسواك والنكاح (سنن الترمذي، الرقم: ١٠٨٠) قال أبو عيسى: حديث أبي أيوب حديث حسن غريب

About admin

Check Also

Fadhila za Jumu’ah

Kusamehewa Madhambi Kwa Kuswali Jumu’ah Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu …