Dua Unapo Ota Ndoto Mbaya

Ikiwa unahofu usiku kwa sababu ya kuona ndoto mbaya, basi soma dua zifuatazo:

Dua Ya Kwanza

أَعُوْذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ الَّتِيْ لَا يُجَاوِزُهُنَّ بَرٌّ وَلَا فَاجِرٌ مِنْ شَرِّ مَا يَنْزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيْهَا وَمِنْ شَرِّ مَا ذَرَأَ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمِنْ شَرِّ فِتَنِ اللَّيْلِ وَفِتَنِ النَّهَارِ وَمِنْ شَرِّ طَوَارِقِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ إلَّا طَارِقًا يَطْرُقُ بِخَيْرٍ يَا رَحْمٰنْ

Naomba kujikinga na maneno kamili ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), ambayo mchamungu wala muovu hawezi kuyapita; najikinga na shari yoyote inayoteremka kutoka mbinguni na inayopanda kwenda mbinguni, na najikinga na shari yoyote alichokiumba duniani na kinachotokea humo, na najikinga na mitihani za usiku na mitihani za mchana, na shari za viumbe wanaotoka usiku na mchana, isipokuwa wale wanaokuja kwa kheri, Ewe Mwingi wa Rehma.

Dua Ya Pili

اَللّٰهُمَّ رَبَّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَمَا أَظَلَّتْ وَرَبَّ الْأَرْضِيْنَ وَمَا أَقَلَّتْ وَرَبَّ الشَّيَاطِيْنِ وَمَا أَضَلَّتْ كُنْ لِيْ جَارًا مِّنْ شَرِّ خَلْقِكَ أَجْمَعِيْنَ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيَّ أَحَدٌ مِّنْهُمْ أَوْ أَنْ يَّطْغٰى عَزَّ جَارُكَ وَتَبَارَكَ اسْمُكَ

Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala), Mola wa mbingu saba na vilivyo kuwa chini ya kivuli chake, na Mola wa ardhi (saba) na viumbe vyote vinavyobeba (juu yake), na Mola wa Mashetani na wale wanao poteza wengine, uwe mlinzi wangu (na unilinde) na shari ya viumbe vyako vyote, ili yoyote miongoni mwao anayevuka mipaka katika kushughulika na mimi au kunidhuru. Ulinzi wako ni mkuu na jina lako limetukuka.

Dua Ya Tatu

أَعُوْذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِن غَضَبِهِ وَعِقَابِه وَشَرِّ عِبَادِهِ وَمِنْ همَزَاتِ الشَّيَاطِيْنِ وَأَنْ يَحْضُرُوْنْ

Naomba kujikinga na maneno kamili ya Allah (Ta’ala) kutoka Ghadhabu yake, na adhabu yake, na maovu ya waja zake, na kutoka kwa sauti ya mashetani na kuhudhuria kwao.

Dua Ya Nne

لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الْعَزِيْزُ الْغَفَّارُ

Hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (Ta’ala) ambaye ni Mmoja, Mwenye nguvu, Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani, Mwenye nguvu kamili na Mwenye kusamehe.

Kumbuka: Dua hii inapaswa kusomwa wakati mtu anaamka kutoka usingizini usiku.

About admin

Check Also

Sunna na Aadaab Za Kulala 3

8. Usilale juu ya tumbo lako. Ya’eesh Ghifaari (Radhiyallahu anhu) anaripoti: Wakati mmoja, nilikuwa nimelala …