Dua Na Adhkaar Kabla Ya Kulala

Dua Ya Kwanza

اَللّٰهُمَّ بِاسْمِكَ أَمُوْتُ وَأَحْيٰى

Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), kwa jina lako nitakufa na kuishi.

Dua Ya Pili

اَللّٰهُمَّ قِنِيْ عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ عِبَادَكَ

Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), niokoe na adhabu Yako siku ambayo utawafufua waja zako (kutoka kaburini).

Kumbuka: Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa akisoma dua hii mara tatu.

Dua Ya Tatu

اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ الَّذِيْ أَطْعَمَنَا وَسَقَانَا وَكَفَانَا وَآوَانَا فَكَمْ مِمَّنْ لَا كَافِيَ لَهُ وَلَا مُؤْوِيَ

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala), aliyetupa chakula, vinywaji, akatutimizia haja zetu na akatupa sehemu pakulala. Kuna wengi ambao hawana mtu wa kuwasaidia, wala hakuna wa kuwapa sehemu ya kulala.

Dua Ya Nne

أَسْتَغْفِرُ اللهَ الَّذِيْ لَا إِلٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّوْمُ وَأَتُوْبُ إِلَيْهْ

Naomba msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), ambaye hakuna apasae kuabudiwa isipokuwa yeye, Aliye hai, Msimamizi wa kila kilichopo, na ninarejea kwake kwa toba.

Kumbuka: Fadhila ya kusoma dua hii ni kwamba dhambi zote ndogo za mtu zitasamehewa.

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’id (Radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema kwamba mtu anayesoma haya yaliyotajwa hapo juu mara tatu kabla ya kulala, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala)Atamsamehe madhambi yake (madogo), hata yakiwa mengi sawa sawa na povu la bahari, majani kwenye mti, chembe za mchanga katika Aalij (sehemu jangwani yenye lundo la mchanga mwingi), na sawa sawa na siku za dunia.

About admin