16. Ni mustahab kufanya qailoolah (kulala mchana kidogo), kwa sababu hii itakusaidia kuamka Tahajjud.
Ibnu Abbaas (Radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Jisaidieni na saumu mchana kwa kula daku, na jisaidieni na kusimama tahajjud usiku kwa kulala mchana (qailoola).”
17. Hakikisha kwamba unaswali, unajishughulisha na dhikr au kufanya jambo lolote jema kabla ya kulala, ili kama kifo chako kimeandikwa kuwa usiku huo, kitendo chako cha mwisho kiwe ni kitendo cha haki na cha uchamungu. Hakikisha kwamba hutendi dhambi au tendo lolote baya kabla ya kulala.
Jaabir (Radhiyallahu anhu) anaripoti kuwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Mtu anapolala, Malaika na Shetani humjia. Malaika anamuombea dua akisema, ‘Mwisho wako uwe juu ya kheri,’ na Shetani husema, ‘Mwisho wako uwe juu ya shari.’ Akimkumbuka Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) kisha akapitiwa na usingizi, Malaika hupitisha usiku wote kumlinda na kumlinda na aina yoyote ya shari.”
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu