14. Ukiona ndoto nzuri, basi sema Alhamdulillah. Unaweza kumsimulia mtu ambaye ana ujuzi katika tabiri za ndoto au kwa mtu ambaye ni mkutakia mema.
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’eed Khudri (Radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mmoja wenu akiona ndoto nzuri inayomfurahisha, basi ahesabu hiyo ndoto kuwa ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala). Baada ya hapo amtukuze Allah Ta’ala na anaweza kumsimulia ndoto hiyo kwa mtu ambaye anaujuzi wakutabiri ndoto au kwa mtakia mema). Lakini, ikiwa mtu anaona ndoto mbaya, basi aichukulie ndoto hiyo kuwa ni kutoka upande wa Shetani, na aombe ulinzi wa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake na asimtajie mtu yoyote ndoto hiyo, kwa sababu ubaya wa ndoto hiyo hautamletea madhara yoyote.”
15. Ukiona ndoto mbaya basi iga kitendo cha kutema mate upande wako wa kushoto mara tatu na usome dua ifuatayo mara tatu. Baada ya hayo, unapaswa kubadilisha jinsi ya kulala. Pia ni bora kufanya wudhu na kuswali. Haupaswi kumsimulia mtu yoyote ndoto mbaya yenye umeiona.
أَعُوْذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيْمِ
Jaabir (Radhiyallahu anhu) anasimulia kuwa Mtume (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mtu anapoona ndoto mbaya basi aige kitendo cha kutema mate ubavu wake wa kushoto mara tatu, kisha aombe ulinzi wa Mwenyezi Mungu mara tatu kutoka kwa shetani na kubadilisha nafasi yake ya kulala.” (Katika riwaya nyingine ya Swahih Muslim, imetajwa kuwa mtu anatakiwa kutawadha na kuswali.)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu