Wakati Abu Dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokaribia mwisho wake, hapakuwa na mtu yoyote pamoja naye isipokuwa mke wake na mtumwa wake. Akawausia akisema, “Nipeni ghusl na nifunike ndani ya sanda (yaani baada ya mimi kufariki dunia). Kisha chukueni mwili wangu na kuuweka njiani, mwambieni msafari wa kwanza anapopita, “Huyu ni Abu Dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu), swahaba wa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam). Tusaidieni kumzika.”
Alipofariki, wote wawili walifanya kama alivyowaagiza (yaani walimpa ghusl na kumfunika sanda na kisha wakauweka mwili wake barabarani).
Msafara wa kwanza kupita ulikuwa ni msafara wa Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu). Yeye alikuwa akielekea Makka Mukarramah kufanya Umra akifuatana na watu fulani kutoka Iraq.
Walipokuwa wakipita walishangaa kuona mwili ukiwa umelala njiani na kuhofiwa kwamba ngamia wangeukanyaga. Katika hatua hiyo, mtumwa wa Abu dhar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alijitokeza na kuwaambia watu wa msafara huo, “Huu ni mwili wa Abu dhar, swahaba wa Nabii (Sallallahu alaihi wasallam) tusaidieni tumzike.
Aliposikia hayo, Abdullah bin Masoud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alianza kulia na kusema, “Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema ukweli aliposema (katika hafla ya Tabook), “Ewe Abu dhar! Unatembea peke yako (kuungana nasi kwa msafara wa Tabuk), utapita peke yako na utafufuliwa peke yako.”
Kisha wakashuka kutoka ngamia yao na kwenda kumzika. (Ibn Sa’d 4/177)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu