Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) Akisifu Kisomo cha Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwahi kusimulia tukio lifuatalo:

Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa akiongea na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) baada ya Esha na kujadiliana naye mambo ya Waislamu. Usiku mmoja, baada ya Esha, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alizungumza na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) (kuhusu mambo ya Waislamu) na mimi pia nilkuwepo pamoja nao. Baada ya kujadiliana, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisimama na kuondoka nyumbani kwake Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) nasi pia tukaungana naye.

Tulipokuwa tukitembea, tulipita karibu na msikiti, na kisha tukasikia sauti ya mtu akisoma Qur’an Majeed ndani ya swalah msikitini. Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisimama kusikiliza kisomo cha Sahaabi huyo. Tulikuwa hatuna uhakika ni nani anayesoma mpaka Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akatuambia:

من سره أن يقرأ القرآن رطبا كما أنزل فيقرأه على قراءة ابن أم عبد

“Mwenye kutaka kuisoma Qur’an Tukufu kama jinsi ilivyoteremshwa (kutoka kwa Mwenyezi Mungu), basi aisome (Qur’an) kama jinsi Abdullah bin Mas’uud anavyoisoma.”

Baada ya hapo, Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikaa chini akikamilisha Swalah yake, kisha akashiriki katika dua. Alipoanza dua yake, kwanza alimtukuza Allah Ta’ala, kisha akamswalia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), kisha akaanza kumuomba Allah Ta’ala mahitaji yake. Aliposikia namna alivyoomba dua (yaani kwa kumhimidi Allah Ta’ala na kumswalia mtume kabla ya kuwasilisha haja zake), Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema mara mbili: “Omba!
chochote unachotaka, hakika utapewa ulichoomba.”

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) hakusikia kile ambacho Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alichokisema kuhusiana na usomaji wake wa Quraan Majeed na dua yake kukubaliwa na Allah Ta’ala.

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajisemea: “Hakika nitakwenda kukutana naye asubuhi na kumpa bashara ya yale aliyoyataja Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kuhusu yeye.

Asubuhi iliyofuata, Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikwenda kwake kumpa bashara, lakini alipofika nyumbani kwake, alimkuta Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) tayari anatoka nyumbani kwa Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu). Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliingia nyumbani kwa Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kumjulisha bashara njema lakini Abdullah bin Mas’uud alimwambia: “Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) ametoka kunijulisha sasa hivi (kabla hujaja).”

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kisha akasema, “Mwenyezi Mungu amjalie rehema zake maalum Abu Bakr! kila nikitaka kumshinda katika kheri ananishinda kila wakati!

Imepokewa katika baadhi ya riwaya kwamba Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) pia alimuuliza Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni dua gani aliyoiomba usiku.

Abdullah bin Masuud akamwambia, “Dua niliyoiomba usiku ilikuwa,

اللهم إني أسألك إيمانا لا يرتد، ونعيما لا ينفد، ومرافقة محمد في أعلى جنة الخلد

Ewe Mwenyezi Mungu, nakuomba unijaalie Imaan ambayo baada yake hakuna kurudi nyuma, na unibariki kwa fadhila ambazo hazitakwisha, na unijaalie niwe na Nabii Muhammad (Sallallahu alaihi wasallam) katika daraja za juu kabisa za Jannah (Akhera) ambayo maisha yake yataendelea milele.

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) pia alitaja dua ifuatayo aliyoiomba baada ya kuswali usiku:

اللهم لا إله إلا أنت، وعدك حق، ولقاوك حق، وكتابك حق، والنَّبيُّون حق، ومحمد صلى الله عليه وسلم – حق والجنة حق والنار حق، ورسلك حق

Ewe Mwenyezi Mungu! Hakuna mungu ila Wewe, ahadi Yako ni haqi, kukutana kwetu na Wewe (Akhera) ni haqi, Kitabu chako (Qur’an Majeed) ni haqi, manabii wote ni haqi, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) ni wa haqi, Jannah ni haqi, Jahannum ni haqi na Mitume wako wote ni wa haqi. tunaamini kuwa yote ni haqi).

(Musnad Abi Ya’la #194, Musnad Ahmad #4338, Sunan Tirmizi #593, Majmauz Zawaaid #15551 & 15557)

About admin

Check Also

Heshima Kubwa Abu Dhar (Radhiyallahu ‘Anhu) Alikuwa Nayo Kwa Uthmaan (Radhiyallahu ‘Anhu)

Mtu kutoka katika kabila la Banu Sulaym alisimuliya yafuatayo: “Wakati mmoja nilikuwa nimekaa kwenye mkutano …