Dua ya sita
Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala), ambaye analisha na yeye halishwi. Alitupa neema zake kisha akatuelekeza kwenye njia sahihi, na akatupa chakula na vinywaji, na kila neema nzuri - alitupendelea nayo. Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala), ambaye alitupa (sisi) chakula, akatupa (sisi) vinywaji, akatuvisha (sisi) kutoka katika hali ya kuwa uchi, ambaye alituelekeza (sisi) na kutuondoa (sisi) kutoka upotovu, alitupa macho na kutuondoa (sisi) katika hali ya upofu na akatupendelea (sisi) zaidi ya viumbe vyake zingine. Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala), Mola wa ulimwengu.
Soma Zaidi »
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu