Sunna na Adabu za kabla ya kula 4

8. Wakati wa kula, mtu hapaswi kukaa kimya kabisa. Lakini, mtu hapaswi kuongelea mambo ambayo yatasababisha wengine kukereheshwa, kupta kichefuchefu au kupoteza hamu ya kula (k.m. kuongea kuhusu mtu kufa, kuumwa nk).

9. Ikiwa unakula na wengine na chakula ni kidogo, basi uwe mstaraabu na uhakikishe kuwa wengine pia wanaweza kula.

Sunna na Adabu za baada ya kula

1. Baada ya kula, safisha vizuri sahani yako au chombo chochote ambayo unakulia kama (bakuli, nk). Inaripotiwa katika Hadith kwamba sahani huwaombea dua ya msamaha kwa yule anayeisafisha baada ya kula.

2 baada ya kula, lamba vidole vyako. Kwanza lamba kidole cha kati, kisha kidole cha shahaadah, na mwishowe kidole gumba.

Abu Hurairah (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Pindi mnapokula chakula, basi unapaswa kulamba vidole vyenu, kwa sababu haujui ni chakula gani kilicho na baraka maalum za Allah Ta’ala.”

3. Soma dua ifuatayo baada ya kula:

اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ الَّذِيْ أَطْعَمَنَا وَسَقَانَا وَجَعَلَنَا مُسْلِمِيْنَ

Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) aliyetupa chakula na vinywaji na kutufanya sisi kuwa miongoni mwa Waislamu.


 

About admin

Check Also

Kula

Dini ya Uislamu ni Dini ya dunia nzima. Ni kwa nyakati zote, maeneo yote na …