Wakati Sa’eed bin Zaid (Radhiyallahu ‘Anhu) alipofariki, sa’d bin abi Waqqaas (Radhiyallahu’ Anhu) na Abdullah bin Umar (Radhiyallahu ‘Anhuma) walikuwa miongoni ya watu waliompa Ghusal.
Baada ya Janazah kubebwa na watu kutoka Aqeeq kwenda Madinah Munawwarah kuzikwa huko Baqi ‘, kaburi la Madinah Munawwarah. Pindi Janaazah ilipopita nyumba ya Sa’d (Radhiyallahu anhu), Sa’d (Radhiyallahu anhu) alingia nyumbani kwake kuoga kabla ya kujiunga na watu katika janazah.
Kabla ya kuondoka nyumbani kwake, aliwambia familia yake kw kusema, “Sikuoga kwa sababu nilishiriki katika Ghusal ya Sa’eed (Radhiyallahu ‘Anhu). Badala yake, nilioga tu kwa sababu ya joto.” (Majmauz Zawaaid, #14880)