Kuhusu Sisi

Allah subhaana wata’ala amesema katika qur ani tukufu:

اليوم اكملت لكم دينكم واتممت عليكم نعمتى ورضيت لكم الإسلام دينا

Siku ya leo nimewakamilishia dini yenu na nimetimiza ahadi zangu kwenu na nimeridhia kwenu dini ya uislaam (surah maaidah v.3)

Aya hii imeteremshwa wakati wa hajjatul wadaa ( hajji ya mwisho). Katika aya hii, tumefahamishwa kwamba dini yetu ya uislaam imekamilika. Dini ya uislaam ni dini pekee ambayo inakubalika na inapendwa kwa Allah subhaana wata’alah na itabaki kiasili mpaka siku ya mwisho.

Kila zama na kila kipindi, Allah subhaana wata’alah alikuwa anachaguwa watu muhimu kwa ajili ya utunzaji na kulinda uislaam. Hawa watu muhimu wamesambaza ufundishaji wa qur ani na hadith na kurekebisha aqida ( yaani imani) za uislaam kwa watu. Wamefanya juhudi kubwa kusambaza dini iliyo kamilika kwa ummah kama ilivyoteremshwa hapo nyuma, jinsi ilivyo teremshwa kutoka kwa maswahaba (radhiyallahu ‘anhum), taabi’een (rahimahumullah), na wachamungu wazamani.

Hii website ina lengo na madhumuni sawa na hayo kufikisha kwa ummah usahihi na ufundishaji mzuri wa uislaam ambao uko imara kutoka kwa vyanzo halisi vya dini. Tunaomba Allah subhaana wata’alah akubali juhudi hizi dhaifu na afanye iwe sababu ya ummah kupata manufaa kamili Aameen.

Ifaamike kwamba website hii iko chini ya uongozi wa Mufti Ebrahim Salejee ( mudiri wa chuo cha Ta’leemuddeen, Durban, Isipingo Beach).

Habari Fupi Ya Kuhusu Mufti Ebrahim Salejee

Mufti Ebrahim Salejee alimaliza masomo yake katika chuo cha deoband (india) na nikhalifa mkuu wa Moulana Maseehullah khan (rahimahullah) wa Jalalabad (India) na Mufti Mahmoodul Hasan (rahimhullah) wa Gangoh.

Katika chuo cha deoband, alikuwa amejaliwa kusoma chini ya walimu wa kubwa kama Qari Tayyib, Mufti Mahmoodul Hasan, Moulana Anzar Shah Kashimeeri (rahimahumullah) na wengineo.

Mufti Ebrahim Salejee amejaliwa na Allah subhaana wata’alah kutowa huduma kubwa katika kazi za tazkiya (marekebisho na usafishaji nyoyo ambazo mtu kuingia kwenye dini kamilifu) zaidi ya hapo, kuna mamia ya madrasah za maktab na taasisi za dini na kuna depatiment ambazo ziko chini ya uongozi wake na usimamizi wake.

Watu wengi wamefanya mahusiano wenyewe kwa Mufti Ebrahim Salejee kwa sababu ya kufanya islaahi na kujirekebisha wenyewe. Mara kwa mara wanahudhuria majlisi (mawaidha) za kila wiki juu ya mada kuhusu usafishaji nyoyo mada zingine zinazohusika, ambapo zina uwezo wa kupa imani nguvu na uboresho wa maisha yao.

Baada ya kumaliza kutoka chuo cha Deoband, Mufti Ebrahim Salejee alirudi South Africa sehemu ambayo alianzisha madrasah inayoitwa Ta’leemuddeen katika nyumba yake. Alhamdulilah, leo hii madrasah inahesabika miongoni mwa madrasah maarufu katika africa kusini, mamia ya wanafunzi wanapata elimu ya dini kutoka madrasah. Baada ya hapo wanasambaza elimu ya dini dunia nzima.

Tunaomba dua kwa Allah subhaana wata’alah amjalie Mufti Ebrahim Salejee afya na ampe maisha marefu, na ummah uweze kuendelea kupata faida kwake. Aamin.