Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) amesema "yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara kumi, Allah subhaana wata'alah atatuma salaam kwake mara mia moja, na yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara mia moja, Allah subhaana wata'alah atamtumia salaam kwake mara elfu moja, na yoyote atakaye zidisha (kunisalia mimi) kwa ajili ya upendo (kwa ajili yangu) na kwa hamu (kwa ajili ya kutafuta thawabu), nitamuombea na nitakuwa shahidi kwa ajili yake siku ya mwisho".
Soma Zaidi »Monthly Archives: April 2021
Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 4
21. Kuna baraka nyingi kwa kuamka muda wa daku. Kwa hiyo mtu atimize sunna ya daku kabla kuanza kufunga.
Sayyidina Abuu Sa'eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema daku inabaraka nyingi. Kwahiyo usiache sunna ya daku, hata kama mtu anaweza kunywa tonye moja la maji muda wa daku (inabidi mtu afanye hivyo ili atimize sunna ya daku.) Kwa hakika Allah subhaana wata'alah ananyunyizia rehema zake maalumu juu ya wale ambao wanaamka muda wa daku na malaika wanawaombea dua maalumu).
Soma Zaidi »Kupata dua maluum ya wamalaikah
Aamir bin Rabee'ah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabiii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, "yoyote atakae niswalia, wamalaikah wataendelea kumswalia yeye (yaani: kumuombea dua) kama ataendelea kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Kwa hiyo, imebaki kwa mtu kuamua kama atataka kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) kidogo au kwa wingi."
Soma Zaidi »Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 3
15. Kwenye mwezi wa ramadhaani, jaribu kuzidisha kwa wingi matendo mazuri. Imepokelewa katika hadith kwamba ibada yoyote ile ya nafili (matendo mazuri ya hiyari) yaliyofanyika katika mwezi wa ramadhaani, inamchumia mtu thawabu ya kitendo cha faradhi, na thawabu ya kitendo cha faradhi kilicho fanyika katika mwezi wa ramadhaani kinazidishwa mara sabini
Soma Zaidi »Thawabu ya yule ambae anamswalia Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) pindi anapo sikia jina tukufu la Nabi wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)
Anas Bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, "mtu ambae jina langu limetajwa mbele yake anatakiwa atume salamu juu yangu, na kwa hakika yoyote ambae ananitumia salamu mara moja, Allah subhaana wata'alah atamtumia baraka kumi juu yake."
Soma Zaidi »Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 2
8. Kwa ukaribio wa ramadhaani na pia kwenye ramadhaani, inabidi mtu asome dua ifuatayo
ewe Allah! Nilinde kwa ajili ya ramadhaani, (kwa kunifanya niuone mwezi wa ramadhaani nikiwa na afya na nguvu ili niweze kuchukuwa maximum faida ndani yake,) na nilindie mwezi wa ramadhaani (kwa kufanya ndani yake nipate maximum faida) na unikubalie.
Soma Zaidi »Kutafuta wema kutoka kwa chanzo chake
Abu hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Amesema," yule ambae anasoma quraani tukufu, anamsifu Allah subhaana wata'alah anamswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Na anaomba msamaha kutoka kwa mola wake basi ametafuta wema kutoka kwa chanzo ya kweli za wema(yaani: amefanya matendo ambayo ni chanzo za wema kwake)."
Soma Zaidi »Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 1
1. Anza kujiandaa kabla ya mwezi mtukufu wa ramadhaani. Baadhi ya wachamungu walikuwa wanajiandaa miezi sita kabla ya ramadhaani.
2. Pindi mwezi wa rajabu unapoanza, soma dua ifuatayo
Soma Zaidi »Kupata Thawabu Sabini
Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti, "mtu yoyote atakaye mswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) mara moja, Allah subhaana wata'alah na malaika wake watamtumia rehema na baraka sabini juu yake kwa kumrudishia salaam yake ile ile moja. Baada ya hapo mtu yoyote atakae taka kuzidisha salaam zake azidishe, na yoyote atakae taka kupunguza hapunguze (yaani kama anataka kupata thawabu nyingi, basi azidishe salaam zake).
Soma Zaidi »