Kutafuta wema kutoka kwa chanzo chake

عن أبي هريرة قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من قرأ القرآن وحمد الرب وصلى على النبي صلى الله عليه وسلم واستغفر ربه فقد طلب الخير مكانه (شعب الإيمان، الرقم: ٢٠٨٤، وسنده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٨٠)

Abu hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Amesema,” yule ambae anasoma quraani tukufu, anamsifu Allah subhaana wata’alah anamswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Na anaomba msamaha kutoka kwa mola wake basi ametafuta wema kutoka kwa chanzo ya kweli za wema(yaani: amefanya matendo ambayo ni chanzo za wema kwake).”

Salamu kuja kumsaidia mtu baada ya kufa

Qissa ifuatayo imerikodiwa ndani ya Al-Raudhul Faaiq (kitaabu). Sheikhe Sufyaan Thauri (rahimahullah) kaeleza:

kuna wakati moja, wakati nilikuwa na fanya tawafu, nilimuona mtu na yeye akifanya tawafu. Tawafu yake nzima, alikuwa anamswalia tu Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) kila hatua, na alikuwa asomi tasbeeh wala tahleel yoyote n.k.

Pindi nilimuuliza sababu, alijibu,” wewe ni nani?” nilijibu,” mimi ni sufyaan thauri.

“kisha akasema: “lau usingekuwa msomi pekee wa kiwango chako, nisinge funua siri yangu. Mimi na baba yangu tulienda ku hijji. Wakati wa kurudi, baba yangu aliumwa. Wakati nilikuwa na jaribu kila kitu kumuuguza, alifariki ,na sura yake nzima ilibadilika kuwa nyeusi. Hiii ilinisumbua sana kiasi (niligundua hii ni alama mbaya) nikasema ,’inna lillah.’

“kisha nilifunika uso wake na kitambaa. Baada ya hapo baadaye ,macho yangu yalifungwa na nikaenda kulala na huzuni hii. Katika mayoni, nilimuona mtu ananijia. Sijawahi kumuona mtu mzuri kama yeye ,nguo safi kama yake, na harufu nzuri kama yake. Alinijia kwa haraka ,na akaondoa kile kitambaa kwenya uso wa baba yangu ,na akaweka mkono wake kwenye uso wake. Hapo hapo, sura ya baba yangu ilibadilika kuwa nyeupe.

“Alipokuwa karibu kuondoka, nilimshikilia na nikasema.’ Allah subhaana wata’alah awe na rehma juu yako. Nakuomba uniambie wewe ni nani, kwa sababu Allah subhaana wata’alah Alimuonesha rehma baba yangu katika hitaji lake kubwa kwa sababu ya wewe. Akajibu, ‘kwani aunitambui mimi? Mimi ni Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) mtoto wa Abdullah, mtu wa quraani tukufu. Baba yako alikuaa mwenye kufanya madhambi makubwa , lakini alikuwa mwenye kuniswalia kwa wingi. Kwa hivyo, kupitia madhambi yake, maovu yalimshukia, niliona maitaji yake makubwa na nikaharakisha kumsaidia, kama jinsi ninavyo fanya kwa wale wote wanao niswalia.” (Ar Radul Faiq Pg,241)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …