Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 1

1. Anza kujiandaa kabla ya mwezi mtukufu wa ramadhaani. Baadhi ya wachamungu walikuwa wakijianda miezi sita kabla ya ramadhaani.

2. Pindi mwezi wa rajabu unapoanza, soma dua ifuatayo

اَللّٰهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِيْ رَجَبٍ وَّشَعْبَان وَبَلِّغْنَا رَمَضَان

ewe Allah! Tubariki sisi katika mwezi wa Rajab na sha’ban na utufikishe katika mwezi wa ramadhaani.

عن أنسٍ رضي الله عنه قال كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ إذَا دَخَلَ رَجَبٌ قَالَ: اَللّهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِيْ رَجَبٍ وَّشَعْبَانَ وَبَلِّغْنَا رَمَضَان (شعب الايمان، الرقم: 3815)

Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba pindi mwezi wa rajab unapoanza Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa anasoma dua ifuatayo “ewe Allah! Tubariki sisi katika mwezi wa rajab na sha’ban na utufikishe katika mwezi wa ramadhaani.”

3. Fanya ratibaa na upange muda maalumu wa kufanya ibada kama kusoma qur an n.k. kwa sababu kujipanga na kuwa makini katika muda wako, utakuwa umejiepusha na kupoteza muda muhimu Wa ramadhaani.

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه و سلم قال من صام رمضان وعرف حدوده وتحفظ مما ينبغي له أن يتحفظ كفر ما قبله (صحيح ابن حبان، الرقم:3433)

Sayyidina Abuu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “yoyote atakae funga mwezi wa ramadhaani, anatambuwa (na anaheshimu) mipaka yake, na anahakikisha anatimiza haki zake za ramadhaani kama jinsi inavyotakiwa, atasamehewa madhambi yake yote yaliyopita.

4. Kama mtu ana deni lolote ambalo Allah Ta’ala anamdai (mf swalah ya qadhaa, swaum ya qadhaa, zakaah ambayo haijatolewa n.k) au deni ambalo unadaiwa na mtu (kwa mfano amemdhulumu mtu fulani, amemuumiza mtu fulani katika njia yoyote, Au ana deni hajalipa), basi kabla mwezi wa ramadhaani haujaanza, inabidi aweke mambo yake sawa sawa kwa kutimiza madeni zake zote ambazo anadaiwa. Kwa kufanya hivyo, atakuwa na uwezo wa kupata baraka zote za mwezi wa ramadhaani.

5. Jaribu pole pole kuzidisha ibada zako kabla ya ramadhaani na jiingize kwenye ratiba maalum ya kufanya ibada ili itakuwa raisi kufanya ibada katika mwezi wa ramadhaani.

6. Jishughulishe na kuomba msamaha kwa wingi na dua kabla ya mwezi wa ramadhaani.

7. Jaribu kumaliza kazi zote za muhimu kabla ya ramadhaani ili muda wako wote uwe unajishughulisha na ibaada.

عن عبادة بن الصامت رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم قال يوما وحضر رمضان أتاكم رمضان شهر بركة يغشاكم الله فيه فينزل الرحمة ويحط الخطايا ويستجيب فيه الدعاء ينظر الله تعالى إلى تنافسكم فيه ويباهي بكم ملائكته فأروا الله من أنفسكم خيرا فإن الشقي من حرم فيه رحمة الله عز وجل (مسند الشاميين للطبراني، الرقم: 2238)

Sayyidina Ubaabah Bin Saamit (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba kuna wakati mmoja, kabla ya ramadhaani, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwaambia maswahaba (radhiyallahu ‘anhu) “ramadhaani ipo karibu kukufikieni. Ramadhaani ni mwezi wa baraka. Ndani ya mwezi huu Allah subhaana wata’alah anateremsha rahma zake maalum, anasamehe madhambi zenu na anazikubali dua zenu. Allah subhaana wata’alah anawaangalia wanaoshindana kufanya mambo mazuri ndani ya ramadhaani (kwa ajili ya kumrizisha) Allah Subhaana wata’alah anajidai kwa malaika zake kuhusu nyie. Kwa hivyo muonyeshe Allah Ta’ala juhudi zenu za uchamungu na matendo mazuri, kwa hakika mtu ambaye hajafanikiwa ni yule aliyenyimwa rahma za Allah Ta’ala ndani ya mwezi mtukufu.

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …