Kupata Thawabu Sabini

عن عبد الرحمن بن مريح الخولاني قال سمعت أبا قيس مولى عمرو بن العاصي يقول: سمعت عبد الله بن عمرو يقول: من صلى على رسول الله صلى الله عليه وسلم صلاة صلى الله عليه وملائكته سبعين صلاة فليقل عبد من ذلك أو ليكثر (مسند أحمد، الرقم: ٦٦٠٥، وإسناده حسن وحكمه الرفع إذ لا مجال للإجتهاد فيه كما في القول البديع صـ ٢٣٧)

Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti, “mtu yoyote atakaye mswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) mara moja, Allah subhaana wata’alah na malaika wake watamtumia rehma na baraka sabini juu yake kwa kumlipa salaam yake ile moja. Baada ya hapo mtu yoyote atakae taka kuzidisha salaam zake azidishe, na yoyote atakae taka kupunguza hapunguze (yaani kama anataka kupata thawabu nyingi, basi azidishe salaam zake).

Kusamehewa Kupitia Baraka Za Kumswalia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Mchamungu mmoja anaeleza kisa ifuatayo: Niliwahi kumuona mtu mmoja aliejulikana na cheo “Mistah” kwenye ndoto baada ya kufariki. Alikuwa mtu wakufanya madhambi wakati alipokuwa hai. Na nilimuona ndotoni na nikamuuliza, “Ni jinsi gani Allah subhaana wata’alah alidili na wewe?” Alijibu “Allah Ta’ala alinisamehe”. Nilimuuliza, “kwa kupitia kitendo gani?” Alijibu, “kuna wakati mmoja nilimuuliza muhaddith fulani kunisomea hadith na sanad yake mpaka Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam). Wakati alitaja jina uliobarikiwa wa Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam), muhadith huyo alimswalia mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam). Na mimi pia nikamswalia Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa sauti. Wakati niliskika namswalia Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa sauti, watu waliokuwepo kwenye kikao hicho na wao pia walimswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Wakati ule, Allah subhaana wata’alah hakatusamehe dhambi sisi wote. (Al Qurbah Li Ibn Baskuwaal Pg.122)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …