عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا مجالسكم بالصلاة علي فإن صلاتكم علي نور لكم يوم القيامة (الفردوس بمأثور الخطاب، الرقم: ٣٣٣٠، وإسناده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٧٨)
Ibnu umar (radhiyallahu anhuma) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alisema, “Pamba mikusanyiko yenu na kunitumia salaam, kwa sababu siku ya qiyaama, salamu zenu juu yangu itakuwa nuru (sababu ya nuru) kwenu.”
Mahitaji Ya Mtu Kutimizwa
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mtu anaposimama kwenye kaburi langu na akinitumia swala na salaam juu yangu naisikia, na mwenye kunisalimia mahali pengine popote, mahitaji na haja zake zote za duniani na Akhera zitaitimizwa, na siku ya Qiyaamah nitakuwa shahidi na mwombezi kwake.”