Maelezo Ya Nabi Isa (alayhis salaam)

Nabii Isa (‘alaihis salaam) alitumwa na Allah Ta‘ala kwa Bani Israa’il. Miongoni mwa amri ambazo Allah Ta’ala alimpa ni kuwapa watu wake bashara kuhusu kuja kwake Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) duniani. Allah Ta’ala anataja katika Qur-aan Majeed:

Na kumbuka Nabii Isa (‘Alayhis Salaam), mwana wa Maryam (‘alaihas salaam), aliposema: “Enyi Bani Israa’il! Mimi ni Mtume wa Allah (Nimetumwa) kwenu, ninayesadikisha Tawrat (iliyoteremshwa) kabla yangu, na ninabashirie Mtume atakayekuja baada yangu ambaye jina lake ni Ahmad (Sallallahu alaihi wasallam). (Surah Saff aya 6)

Kama jinsi Nabi Isa (‘Alayhis salaam) alivyowafahamisha watu wake kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) atatumwa duniani kabla ya Qiyaamah kama mjumbe wa mwisho wa Allah Ta‘ala, hivyo hivyo Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliufahamisha Ummah wake kwamba kabla ya Qiyaamah, Nabii Isa (alayhis salaam) atatumwa kuuokoa ummah wake kutokana na fitnah ya Dajjaal.

Kuhusiana na maelezo ya Nabii Isa (‘alayhis salaam), Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliufahamisha ummah sifa yake ya kimwili na pia akaufahamisha ummah mavazi ambayo atakuwa amevaa wakati wa kushuka kwake kutoka mbinguni.

Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Nabii Isa (‘Alayhis Salaam) bila shaka atateremka kutoka mbinguni, kwa hiyo, utakapomuona mtambue (kwa maelezo nitakayokupa) ni mtu wa kimo cha wastani, na rangi yake ni nzuri na nyekundu. Atavikwa vitambaa viwili vya njano na itaonekana kwamba kichwa chake kinamelemeta, ingawa hakikulowa na maji.” (Musnad Ahmad #9270)

Katika baadhi ya hadith, imetajwa kuwa rangi ya Nabii Isa (‘alaihis salaam) itakuwa nyeupe. Ngozi yake itakuwa sawa na rangi ya ngano, na tonye la nyekundu ndani yake kidogo. Atakuwa na urefu wa wastani, akiwa na kifua kipana. Nywele zake zitakuwa ndefu kufikia mabega yake. Wakati wa kushuka kwake, atakuwa amevaa vitambaa viwili vya njano na nywele zake zitaonekana kuwa na maji maji.

About admin

Check Also

Uadilifu na Baraka Wakati wa Utawala wa Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Utawala wa Mahdi (Radhiya Allaahu ‘anhu) utakuwa wa uadilifu na wa baraka. Kwa kuwa Mahdi …