Ujuzi Mkuu wa Muaz bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Abu Muslim Khowlaani (rahimahullah) anataja:

“Niliingia msikiti wa Hims na nikaona mkusanyiko wa watu, miongoni mwao walikuwa maswahaba thelathini na mbili wa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) ambao walikuwa wakisimulia hadithi kutoka kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).

Katika mkusanyiko huu alikuwepo kijana ambaye amepaka wanja jichoni na ambaye meno yake yalikuwa yamen’gaa. Alikuwa amekaa amevaa kitamba. Kila mara watu wa mkusanyiko huu walipokuwa wakitofautiana au kutilia shaka jambo lolote la Dini, walikuwa wakirejea kwake, na walikubali neno lake kuwa la mwisho.

Katika baadhi ya riwaya, imetajwa kwamba Abu Muslim (rahimahullah) aliwauliza waliokuwa karibu naye, “Huyu kijana ni nani?” Wakajibu, “Yeye ni Mu’aaz bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu).”

Abu Muslim Khowlaani (rahimahullah) anaendelea kutaja:

“Asubuhi mapema nilipoelekea msikitini nikamkuta Mu’aaz (Radhiya Allaahu ‘anhu) akiswali karibu na nguzo ya msikiti, nikaanza Swalaah yangu karibu naye na pindi alipogeuka kutoa salaam, nilikaa karibu naye kiasi kwamba baina yetu ni nguzo pekee. Tulikaa kimya kwa muda kidogo na nikamuelekea na kusema, ‘Ewe Mu’aaz! Ninakula kiapo kwa jina la Mwenyezi Mungu, ninakupenda moyoni mwangu, si kwa kutaraji kupata faida ya kidunia, wala kwa sababu ya kuwepo uhusiano wa kifamilia na uhusiano baina yetu.

Mu’aaz bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) akauliza, ‘Kwa nini una mapenzi nami moyoni mwako?’ Nikajibu, ‘Mapenzi niliyonayo moyoni mwangu kwako ni kwa ajili ya Allah Ta’ala.’ Muaaz (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, Je, hii ndiyo sababu pekee (ya wewe kunipenda moyoni mwako), nikasema, ‘Ndio, na aapa kwa jina la Allah (hii ni sababu pekee).’ Tena akaniuliza, “Wallahi, je, hii ndiyo sababu pekee (ya kuwa unanipenda moyoni mwako) nikasema, ‘Ndio, na aapa kwa jina la Allah (hii ndiyo sababu pekee).’

Kisha Mu’aaz (Radhiya Allaahu ‘anhu) akaniambia, ‘Ikiwa hii ndiyo sababu pekee ya wewe kunipenda moyoni mwako, basi ukubali bishara njema; kwani nimemsikia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akitaja maneno ya Allah Ta’ala, “Allah Ta’ala anasema, ‘Mapenzi yangu ni ya lazima kwa watu wawili wanaopendana kwa ajili Yangu tu, wanatumia muda kukaa pamoja kwa ajili Yangu tu, wanatembeleana kwa ajili Yangu tu na wanasaidiana na mali wao kwa wao kwa ajili Yangu tu (yaani Allah Ta’ala Anasema kwamba hakika atawapenda na kuwa radhi nao). (Siku ya Qiyaamah,) watakuwa na mimbari za Nur (mwanga), watafurahia kivuli cha Arsh ya Allah Ta’ala na hadi manabii (alaihimus salaam) na Siddeeqeen watakuwa na wivu nao (Musnad Ahmad #22276 & 22030)

Kumbuka: Ingawa manabii na Siddeeqeen watakuwa wa juu zaidi kwenye daraja na malipo, wao (Manabii na Siddeeqeen) wataonyesha furaha juu ya malipo makubwa ambayo Allah Ta’ala atawaruzuku watu hawa kwa ajili ya kupendana tu kwa ajili Yake duniani.’”

About admin

Check Also

Dakika za Mwisho za Mu’aaz bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika Ulimwengu huu

  Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kufa kwa tauni kafa kama shaheed. Wakati wa …